Mchezaji wa simba sc na 
Beki mwenye kasi wa Simba na Timu ya taifa ya Tanzania , Shomari Kapombe amewaondoa hofu mashabiki wa timu ya simba  kuwa, wasiogopeshwe na sare dhidi ya Mwadui FC ambapo amesisitiza kuwa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwao bado upo palepale.

Kapombe alisema kauli hiyo mara baada ya sare ya mabao 2-2 na Mwadui juzi Alhamisi kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Pamoja na kutoka sare hiyo, Simba imebaki kileleni katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 42 huku Yanga wakifuatiwa wakiwa na pointi 37.

Kapombe alisema mashabiki wa Simba wasikatishwe tamaa na matokeo hayo waliyoyapata kwani bado wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Kapombe alisema kikubwa ni mashabiki wa timu hiyo waendelee kuisapoti timu hiyo kwa kuendelea kujitokeza uwanjani kwa ajili ya kuwashangilia ili waendelee kupata matokeo mazuri.


“Ni ngumu kwa timu kuendelea kupata matokeo mazuri kwenye mechi za ligi, kwani wapinzani wetu nao wanajiandaa kupata ushindi ila matarajio yetu ya ubingwa bado yapo palepale.

“Ushindani kama unavyouona wa ligi msimu huu, timu zote zimejiandaa kwa ajili ya kuchukua ubingwa na nyingine kutaka kumaliza ligi katika nafasi nzuri na ndiyo sababu ya sisi kupata sare na Mwadui.


“Kikubwa mashabiki wetu wasikate tamaa baada ya matokeo hayo, tunajua matokeo yamewaumiza lakini watarajie kupata matokeo mazuri kwenye michezo ijayo,” alisema Kapombe.

SOURCE: CHAMPIONI