Hakuna kategoria za virai katika uchanganuzi wa kisintakisia, kubali au kata hoja hii kwa kutumia mifano maridhawa.
Dhana ya kategoria ni pana na imejadiliwa na watalaam mbalimbali ambao wamegawanyika katika pande kuu mbili ambazo ni kundi la wanamapokeo na wanausasa.
Neno kategoria ni neno lenye asili ya kigiriki lenye maana ya uarifu(prediction) yaani sifa kuu ya kiima.
Wanasarufi mapokeo wanaziona kategoria za kisarufi kuwa ni sifa zinazoambatanishwa kwenye aina za maneno. Kategoria hizo ni kama vile kategoria za nafsi, kategoria za njeo, kategoria ya hali, kategoria ya jenda/jinsia, kategoria ya uhusika na kategoria ya ngeli.
Kwa mujibu wa wanausasa wanasema kategoria ni dailojia mbalimbali katika uundaji wa tungo . katika mkabala huu wa kisasa umeonekana kuwa kuna kategoria kuu mbili ambazo ni:
I)kategoria ya kileksika(neno)
II)kategoria ya virai
Kwa mujibu wa swali tutajikita Zaidi katika kuelezea kategoria ya virai. kabla ya kutazama kategoria ya virai ifuatayo ni nmaana ya virai kama ilivyofasiliwa na watalaam mbalimbali:
Massamba na wenzake(2009), wanaon kuwa kirai ni kipashio cha kimuundo chenye chenye Zaidi ya neno moja ambacho hakina muundo wa kiima kiarifu.
Kihore na wenzake(2007), wanasema kuwa kirai kimefafanuliwa kama kipashio cha kimuundochenye neno moja au Zaidi lakini bila uhusiano wa kiima kiarifu. Kwao mahusiano ya kiima kiarifu ni yale yanayoonyesha anaye tenda jambo na tendo linalotendwa, aneye tenda jambo ni kiima na tendo linalotendwa ni kiarifu.
Mfano: mtu mnene/ anachoma nyama.
Kiima kiarifu
TUKI(2011), kirai ni kipashio chenye Zaidi ya neno moja lakini ambacho hakina muundo wa kiima kiarifu.
Fasili zote hizo zina udhaifu. Na udhaifu huo ni kama ifuatavyo:
Kusema kuwa kirai kina Zaidi ya neno moja si kweli kwani hata neno moja linaweza kuwa kirai.
Mfano: kirai kitenzi kinachoundwa na kitenzi peke yake.
Analima ,wanaimba n.k
KT
T
Analima
Vile vile kusema kuwa kirai hakina muundo wa kiima kiarifu si sahihi kwani kuna baadhi ya sentensi ambazo zina kiima ambacho hakijidhihirishi waziwazi.
Mfano: Anaoga
S
KN KT
N T
Q Anaoga
Pia dai la kuwa kirai ni tungo isiyokuwa na kitenzi ndan yake si sahihi kwani upo uwezekano wa kirai kuwa na kitenzi ndani yake.
Hivyo basi kirai ni kipashio cha kimuundo chenye neno moja au Zaidi chenye neno kuu moja.
Kirai kimejikita katika ziadi katika maneno makuu yenye dhima kubwa kisintaksia kama vile nomino, kivumishi, kitenzi, kihusishi, kielezi na kibainishi.hivyo basi aina hizi za maneno yenye dhima kubwa kisintaksia ndio zinatupati aina za virai.
Ufuatao ni ushahidi wa kuwepo kwa kategoria za virai:
Ushahidi wa kimofolojia: kimofolojia kuna maumbo Fulani yanayothibitisha kuwepo kwa kategoria ya virai nah ii inadhibitika kwa kuangalia viambishi vinavyoambikwa kwenye baadhi ya maneno vikionyesha umoja na wingi.
Mfano: baba na mama wanalima
Kiti na meza vimevunjika
Katika sentensi hizi mbili viambishi vilivyopigiwa msititari vikionyesha umoja na wingi vyenye upatanisho wa kisarufi hudhibitisha kuwepo kwa virai vilivyo katika kategoria moja, kwani vinadhihirisha kuwa vitu vyenye hadhi sawa na visivyo na hadhi sawa haviwezi kusimama pamoja na kuwekewa viambishi hivyo vya umoja na wingi.
Ushahidi wa kisemantiki; katika lugha ya Kiswahili kuna utata unaosababisha na miundo ya virai kisemantiki.
Mfano: juma hamthamini rafiki yake mwanahawa
Juma amempigia annet mpira.
Ni dhahiri kuwa kisemantiki kuna utata, kwani kuna maana Zaidi ya moja katika sentensi hizo hapo juu, kwani katika sentensi ya kwanza tunaweza elewa kuwa ;
Mwanahawa ndiye hathaminiki au
Rafiki yake na mwanahawa ndiye hathaminiki.
Ushahidi wa kisintaksia:Ushahidi huu unaonyesha mtawanyo wa virai. Hii inamaana kwamba ukitaka kuhamisha maneno yaundayo virai, hauna budi kuhamisha kirai kizima na si sehemu tu ya kirai hicho, kudondosha au kuunganisha kirai kizima
Mfano: simuwezi dada yako mkubwa.
Dada yako mkubwa simwezi.
Simpendi kaka yako mkorofi.
· Mkubwa simwezi dada yako.
· Mkorofi kaka yako simpendi.
Kuunganisha virai vyenye hadhi sawa.
Mfano: i) baba analima
Mama analima
Baba na Mama wanalima.
ii) John anasoma
kiti kimevunjika
John na kiti vimevunjika/wanasoma
Sentensi II, hazijaleta maana kwa sababu hadhi siyo sawa an sentensi si sahihi.
Vile vile katika ushahidi wa kisintaksia kuna jaribio la kiubadala (replacement) kulingana na baadhi ya wanaisimu akiwemo carnie Andrew(2007)na O’graddy(1996:193-194) wanasema:
Jaribio la kiubadala hujidhihirisha pale baadhi ya maneno huweza kusimama badala ya kirai kizima au kundi la maneno hususani katika kirai nomino na kirai kitenzi ambavyo vinaweza kuwakilishwa na viwakilishi na maneno kama hivyo au hivyo hivyo n.k.
Mfano: i) wanafunzi watavai tai endapo walimu nao watavaa
Ubadala; Wanafunzi watavaa tai endapo walimu watafanya hivyo
ii) wanafunzi watakao soma kwa bidii watafaulu mitihani vizuri
ubadala: wao watakaosoma kwa bidii watafaulu mitihani vizuri
Kwa hiyo si kweli kwamba hakuna kategoria ya virai katika uchanganuzi wa kisintaksia. Kuna kategoria ya virai, na virai hivyo vimejikita Zaidi katika neno kuu ambalo kuna aina mbalimbali za virai ambavyo ni kirai nomino, kirai kivumishi, kirai kitenzi, kirai kielezi, kirai kibainishi na kirai kihusishi.
Ufuatao ni uchanganuzi wa virau Kisintaksia.
1. KIRAI NOMINO.
Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa kwenye nomino au mahusiano ya nomino na neno au mafungu ya maneno.
Miundo ya nomino:
i)Nomino peke yake.
Mfano: Dada ameondoka
N
Juma atarudi kesho.
N
KN
N
Dada/Juma
ii) Nomino mbili.
Mfano. Baba na mama wanalima.
N1 N2
KN
N u N2
Baba na mama
iii) Nomino na Kivumishi kimoja au Zaidi.
Mfano:
Watu watatu warefu wamesimama njiani.
N
KN
N KV
V KV
V
Watu Watatu Warefu
iv) Nomino na kirai kibaishi
Mfano: Mwanafunzi yule anacheza
KN
KN
N KB
B
Mwanafunzi yule
v) Nomino na sentensi
Mfano: Mtoto aliyepotea jana ameonekana.
KN
N S
KN KT
N T KE
Mtoto aliyepotea jana
Vi) Nomino, kivumishi na sentensi.
Mfano:a) msichana mrembo aliyehamia jana amekwenda sokoni.
b) John mrefu aliyekwenda sokoni asubuhi amepata ajali.
KN
N KV
V S
KN KT
N T KE
E
Msichana Mrembo aliyehamia jana
vii) nomino, Kibainishi na sentensi
mfano:a) watoto wengi wanaofaulu masomo ni wanao soma kwa bidii.
b) vijana wengi wanasiofaulu hawasomi sana
KN
N KB
S
B KN KT
N T KE
E1 E2
Vijana wengi wasiofaulu mitihani yao
2. KIRAI KIVUMISHI.
Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika kivumishi kwa kawaida muundo huo huwa ni wa kivumishi na neno au fungu la maneno linaloandamaana na kivumishi hicho.
Ifuatayo ni miundo ya kirai kivumishi.
a) Kivumishi pekee yake.
Mfano: kiti kizuri
Mtoto mzuri
Kijana mbaya
KN
V
Kizuri
Mzuri
b) kivumishi na kirai nomino.
Mfano: i) mtoto mwenye kelele nyingi
ii)Mwanafunzi mchafu miguu yake
KV
KV KN
N KB
B
Mwenye kelele nyingi
c) kivumishi na kirai kielezi.
Mfano: a)Chungwa baya sana.
b)Mama korofi sana.
c) Mwalimu mpole mno.
KN
V KE
E
Mpole mno
d) kivumishi na sentensi.
Mfano: motto mzuri aliyekuja sana asubuhieondoka.
Maji machafu yaliyotiririka mferejini yananuka.
KN
V S
KN KT
N T KE
E
Machafu yaliyotiririka mferejini
e) kivumishi na kirai kihusishi,
mfano: mme mzuri wa dada anaumwa.
Kilio kikubwa cha watanzania ni maji safi
KV
V KH
H KN
N
Kikubwa cha watanzania
f) Kivumishi na kirai kivumishi
mfano; Simu nzuri nyeusi imeibiwa
Ua zuri jekundu limenyauka
KV
V KV
V
Zuri jekundu
3.KIRAI KITENZI
Ni kirai ambacho mahusiano ndani yake yamekitwa katika kitenzi (Kihore na wenzake 2007) ni kirai ambacho kimekitwa katika kitenzi, hii ina maana kuwa neno kuu katika aina hii ya kirai ni kitenzi(Massamba na wenzake 2009)
Miundo ya virai vitenzi ni kama ifuatavyo
a) Kitenzi peke yake
mfano; Amelala
;Wameamka
KT
T
Amelala
b) Kitenzi na nomino moja
mfano; amempiga juma
ameandika barua
KT
T KN
N
Ameandika barua
c) Kitenzi na nomino mbili.
Mfano; amempa motto chakula
Wanampigia juma kelele
KT
T KN
N1 N2
Amempa mtoto chakula
d) Kitenzi na kitenzi,
mfano; anapenda kutoa
ameamua kurudi
anapenda kusoma
KT
T1 T2
Anapenda kutoa
e) kitenzi, nomino na kitenzi.
Mfano: anamfundisha mototo kusoma
Tuliwataka viongozi kututembelea
KT
T KN
N KT
T
Anamfundisha motto kusoma
f) kitenzi na sentensi
mfano: amesema atarudi kesho
KT
T S
KN KT
N T KE
E
Amesema atarudi kesho
g) kitenzi na kirai kihusishi
mfano: ameondoka kwa basi
anatembea kwa baiskeli
KT
T KH
H KN
N
Anaondoka kwa baiskeli
h) kitenzi, nomino na sentensi
mfano: mwalimu amewambia wanafunzi waende darasani
KT
T KN
N S
KN KT
N T KE
E
Amewambia wanafunzi waende darasani
4. KIRAI KIELEZI
Kirai kielezi ni aina ya kirai ambacho kwacho neno kuu ni kielezi. Kirai hiki kinaweza kuwa na neno kuu
peke yake au kikaambatana na kijalizo chake.
Miundo ya kirai kielezi ni kama ifuatavyo:
a) kirai kielezi peke yake
mfano: jane analimima shambani
peter ameweka kiti chini
KE
E
Shambani
b) kielezi na kielezi kingine
mfano:William anaimba vizuri sana
boom limetoka leo asubuhi
KE
E KE
E
Leo asubuhi
C) kielezi na kirai kihusishi
Mfano: mototo anakula nyumbani kwa watu
Alicheka kwa sauti mkutanoni
KE
E KH
H KN
N
Nyumbani kwa watu
5 .KIRAI KIHUSISHI;
Hii ni aina ya kirai ambayo neno kuu ni kihusishi, mara nyingi kirai kihusishi hakiwezi kuwa na muundo wa kihusishi peke yake hivyo hulazimika wakati wote kuhitaji kijalizo ili kukamilisha maana yake.
Mfano: anazungumza kuhusu mavazi
Juma anakula kuku kwa mrija
Wazurulaji wamekamatwa na polisi.
Miundo ya kirai kihusishi ni kama ifuatavyo:
a) kirai kihusishi na nomino
mfano: amezungumzia kuhusu mavazi
KH
H KN
N
Kuhusu mavazi
b) kirai kihusishi na kitenzi
mfano: jane ameadhibiwa kwa kuimba
juma alipongezwa kwa kufaulu
KH
H KT
T
Kwa kufaulu
c) kihusishi, nomino na kivumishi
mfano :nimechoka kwa matusi yake
ameolewa kwa bwana mzuri
KH
H KN
N KV
V
Kwa bwana mzuri
d) kihusishi, nomino na kibainishi
mfano: wanapendana katika hali zote
mababu zetu waliishi katika bara hili
KH
H KN
N KB
B
Katika hali zote
6.KIRAI KIBAINISHI:
Kirai kibainishi ni aina ya kirai ambayo ni neno kuu huwa ni kibainishi na huweza kuwa peke yake au kuambatana na kijalizo chake.
Miundo ya kirai kibainishi:
a) kibainishi peke yake
mfano :anauza gari lile
mama anafuga ng’ombe wawili
KB
B
Wawili
b) kibainishi na kivumishi
mfano: kajifungua watoto wawili wazuri
amenunua mbuzi wane wanene
KB
B KV
V
Watatu wanene
c) kibainishi na kibainishi kingine
mfano: viwanja hivi viwili ni mali yangu
KB
B KB
B
Hivi viwili
d) kibainishi na sentensi
mfano: mwalimu amewafundisha wanafunzi wale waliokuwa hawajaelewa
kaka yule aliyeigiza na kanumba ni mpare
KB
B S
KN KT
N T1 T2
Wale waliokuwa hawajaelewa
Hivyo basi ni dhahiri kuwa kuna kategoria za virai katika uchanganuzi wa kisintaksia katika lugha ya Kiswahili kwani kwa ushahidi na ubainishaji wa aina mbalimbali za virai na miundo yake twaweza sema kuwa hizi kategoria zipo.
MAREJEO:
Massamba P.B na wenzake (2009) sarufi miundo ya Kiswahili sanifu (SAMIKISA): sekondari na vyuo, TUKI, Dar es salaam.
Kihore M. Y na wenzake (2007) sarufi maumbo ya kiswahili sanifu (SAMIKISA): sekondari na
vyuo,TUKI, Dar es salaam.
TUKI (2011) kamusi ya Kiswahili sanifu. TUKI, Dar es salaam.
Andrew .C. (2007) syntax: a generative introduction second edition; blakwell publishers LTD.USA.
O’graddy .W. (1996) syntax: The analysis of sentence structure; Longman limited. London
Give Your Comment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)