TUMIA JAPO DAKIKA TATU KUSOMA MKASA HUU WA KUSIKITISHA
Huyu kijana anaitwa Benson, Benson alitoka kijijini kwao miaka mitano iliyopita na kuja mjini katika harakati za kutafuta maisha. Alibahatika kupata kazi ya ulinzi katika Shirika moja lisilokuwa la kiserikali na kuaminiwa sana.
Aliweza kuwasaidia wazazi wake kwa hali na mali, kwani alikuwa ni mtoto wa kiume pekee katika familia yao yeye watoto wawili, Benson na mdogo wake wa kike aitwaye Neema.Hivyo alikuwa anawatumia kiasi fulani cha fedha kila alipopokea mshahara wake. Huo ndio ulikuwa utaratibu wake kila mwezi.
Miezi miatau iliyopita alipokea taarifa ya kifo cha Baba yake huko kijiji. Alipoomba Ruhusa ya kwenda kumzika baba yake, Mkurugenzi alimnyima ruhusa. Kutokana na Uchungu wa kupoteza mzazi wake Benson alifikia hatua ya kuzozana no bosi wake huyo na hatimaye kuamua kuondoka kwenda kuzika bila ya kupata ruhusa kazini kwake. Alikaa kule kijijini kwa muda wa wiki moja akarudi kazini lakini huku nyuma familia ile ikimtegemea yeye.
Aliporudi kazini Mkurugenzi wake alimtengenezea kesi ya wizi na upotevu wa mali mbalimbali za kampuni zenye thamani ya Tshs 5,000,000/=(milioni tano) hivyo alifukuzwa kazi bila kupata malipo yoyote.
Ni miezi mitatu sasa toka alipofukuzwa kazi, Benson aliishi kwa uzoefu tu wa mjini akisaidiwa na marafiki.
Hivi juzi asubuhi alipokea taarifa kuwa mama yake ni mgonjwa sana huko kijijni, hivyo zilihitajika fedha kwa ajili ya kumpeleka hospitali. Benson alihangaika kutafuta msaada hata kujaribu kukopa lakini kila aliyemwendea alishindwa kumsaidia kwa chochote.
Jana aliamka asubuhi mapema huku akili na mawazo yake yakiwa kijijini kwa mama yake. Aliamua kwenda kutafuta japo kibarua kitakachompatia japo pesa kidogo ili aweze kuwatumia kijijini waweze kumpeleka mama yake hospitalini.
Katika mizunguko yake alibahatika kupata kibarua cha kupanga bidhaa kwenye ghala ya duka moja kubwa hapa jirani akiwa na wenzake watatu.
Wakati wakiendelea na kazi, mwenzake mmoja ambaye alikuwa mzoefu pale alimwambie achukue boksi moja la sigara aliweke Uchochoroni, Bila ya kutafakari na kutokana na shida ya fedha aliyokuwa nayo wakati ule, Benson alifanya kama alivyoelekezwa.
Wakati analiweka lile Boksi, Mara mtoto wa tajiri alimwona na kuanza kumhoji, Benson alishindwa kujitetea, Ndipo yule mtoto alipoanza kumpigia kelele za mwizi.
Kama ujuavyo jiji hili, Benson alipokea kipigo kikali kutoka kwa watu wenye hasira. watu walianza kumpiga kwa mawe, matofali,na silaha mbalimbali hadi kupelekea kuwa katika hali hii.
Masikini kijana Benson amepoteza maisha wakati kijijini wakisubiria msaada wake ili waweze kumpeleka mama yake hospitali.
Tumwombe mungu atusaidie kwa kila hali nakukaribisha kurudi tena na kusoma MASSHELE BLOG BLOGU YA WATU COMMENT , Lakini pia SHARE NA MARAFIKI WAWEZE KUJIFUNZA CHOCHOTE HAPA.
Kama stori yoyote nitaichapisha Huyu kijana anaitwa Benson, Benson alitoka kijijini kwao miaka mitano iliyopita na kuja mjini katika harakati za kutafuta maisha. Alibahatika kupata kazi ya ulinzi katika Shirika moja lisilokuwa la kiserikali na kuaminiwa sana.