Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kufuta mpango wa "Green Card" baada ya shambulizi la kigaidi lililotekelezwa Manhattan mjini New York ambapo watu waliuawa.
Mshambuliaji ambae alitumia gari dogo la mizigo kugoga watu waliokuwa wakitembea kwa miguu alikamatwa muda mchache baada ya kutekeleza shambulizi hilo ambalo watu wanane walifariki.
Mshambuliaji alitambulika kwa jina la Sayfullo Saipov aliingia mchini Marekani mwaka 2010 baada ya kupata "Green Card" ambao ni mfumo wa Marekani unaorahisisha raia wa kigeni kuingia nchini Marekani na baadae kupata uraia.
Sayfullo aliingia nchini Marekani akitokea nchini Kirghistan.
Rais Trump amesema kuwa gaidi huyo anaweza kupelekwa katika kisiwa cha Guantanamo.
Trump amesema pia kuanzia sasa atashirikiana na baraza la seneti kufuta mpango huo wa Green Card. Kwa mujibu wa rais Trump mpango huo ulikuwa ukifurahisha masikio ya watu na sio taifa la Marekani.