Saturday

HAKIKA TUTAKUKUMBUKA KOCHA JOEL BENDERA

0 comments

Mwili wa Mwanamichezo na Mwanasiasa Joel Nyaka Bendera umeagwa leo kwenye Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Wadau mbalimbali wa michezo wakiongozwa na Rais wa zamani wa TFF, Leodeger Tenga wamejitokeza kumuaga Bendera wakianzia na jumuiya iliyofanyika nyumbani kwake Sinza.

Mwili wa Bendera aliyewahi kuwa Kocha wa Taifa Stars na baadaye Simba, umesafirishwa kwenda mkoani Tanga kwa mazishi ambayo yanatarajiwa kufanyika kesho.

Hadi anafariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili siku nne zilizopita, Bendera alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.


MASSHELE BLOG  INATOA POLE KWA WAFIWA KUANZIA FAMILIA YAKE NA FAMILIA YOTE YA WANAMICHEZO.

MWENYEZI MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA.