Friday

VPL: Wanankurukumbi watia maguu jijini Mbeya, kuwakabili wanakomakumwanya

0 comments


Kikosi cha timu ya soka ya Kagera Sugar ‘Wanankurukumbi’ kimewasili jijini Mbeya tayari kabisa kufanya maandalizi mepesi kuelekea mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Wanakomakumwanya Mbeya City.
Katibu mkuu wa klabu ya Kagera Sugar Hussein Madaki amesema kikosi hicho kipo katika hali nzuri na kwamba wanatarajia kupata ushindi katika mchezo huo ambao utafanyika Jumatatu ya Januari 1, 2018 kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.
-Timu imewasili jijini Mbeya jioni hii, kuhusu mchezo tumejiandaa vizuri kwani tunaamini kuwa hii ni mechi ngumu lakini ni mechi ambayo tunahitaji pointi tatu, na tutajitahidi kuhakikisha tunapata ushindi,” Madaki ameeleza.
Amesema wanaenda kwa kucheza na Mbeya City kwa tahadhari kubwa ukizingatia timu wanayokutana nayo ni timu zoefu kwenye ligi lakini pia ni timu ngumu lakini kwa kuwa lengo lao ni kupata pointi tatu basi watasahau yote hayo na kupambana kwa juhudi.
Kagera Sugar wanakwenda kucheza na Mbeya City katika nafasi ya 10 kwa kukusanya alama 11 ili hali wapinzani wao wakiwa nafasi 12 kwa kukusanya alama 11 ili wakizidiwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Juma Kaseja.
Tayari mlinda mlango wa timu hiyo mkongwe Juma Kaseja amejiunga na timu hiyo akitokea kwenye timu ya Taifa ya Tanzania Bara ambayo ilikuwa ikishiriki michuano ya Soka la Ufukweni iliyomalizika kwa Zanzibar kutwaa ubingwa.
Michezo mitano iliyopita ya Kagera Sugar.
Kagera Sugar 0-0 Stand United
Mtibwa Sugar 0-1 Kagera Sugar
Kagera Sugar 1-1 Tanzania Prisons
Kagera Sugar 2-1 Ndanda FC
Mwadui FC 1-1 Kagera Sugar