Tabia ya uongo imekuwa ni ya hali ya kawaida sana katika orodha ya sifa hasi, hakuna mtu anaependa kujua kama amedanganywa, Lakini ni jambo ambalo karibu sisi sote hufanya mara kwa mara.Kulingana na patterson mwandishi wa “siku ya america kuongea ukweli” kati ya wamalekani elfu mbili asilimia tisini na moja (91%) hudanganya mara kwa mara nyumbani na kazini. Inashangaza sana.
Watu wengi huamua kutudanganya kwa faida yao binafsi au pamoja na wapendwa wao, lakini je unapenda kudanganya kwa kiasi kikubwa ili kulinda hisia zako kutokana na kuumizwa? kama ni hivyo hautumii busara.
Je ufanye nini ili kugundua kama umedanganywa?
linapokuja swala uongo huwa ni vigumu kutambua maana hutumia maneno mara nyingi, hapa nimekuandalia jinsi unavyoweza kuzitambua ishara za mtu anaekudanganya.
Katika kugundua dalili, vitendo huzungumza kweli kuliko maneno kwa sababu vyote hivi ni ishara za mtu mdanganyifu, maneno huwa hayakubaliki moja kwa moja, ili kugundua ukweli unapaswa kuzingatia lugha ya mwili ambayo husaidia sana kumgundua muongo.
Utafiti umegundua kwamba watu hutabasamu kidogo wakati wanapodanganya.
Hasa kwa wanaume, katika utafiti wake paul ekman alithibitisha kwamba watu uhusisha uongo na tabasamu hivyo kuingia katika vitu viwili, kama mtu hatatabasamu anapoongea uongo inamaana hukaribia kusema kweli ila anapoingiwa na wasiwasi
huanza kukuna shingo zao.
Namna nyingine ni pale ambapo mtu anakuna shingo upande wa karibu na sikio, hii hufanywa kwa namna fulani (kwa kutumia kidole cha shahada). Hii ni ishara ya kawaida ya mashaka na kutokuwa na uhakika na jambo husika kwa mtu asiekwambia ukweli wote
hupenda kugusa nyuso zao
Kuleta mkono usoni hii ni njia nyingine ya kawaida ya mdanganyifu, hii inaweza kuwa kwa kufunika macho yao, kuweka mkono kwenye paji la uso au shavu na uwezekano mkubwa unatokana na sifa za utoto. Watoto mara nyingi hufunika kinywa, hufunika masikio yao, hufunika macho yao ili kuacha kuzungumza, kuacha kuongea au kuacha kuona. Hizi daima huwa ndogo, lakini tunapokuwa wakubwa ishara hizi zinazidi kwa haraka na zisizo wazi bado zinatumiwa kidogo
Sio mara zote huonyesha uongo wa hali ya juu, hata hivyo inaweza kumaanisha mtu anahifadhi maelezo ambayo kwa baadhi yanaweza kuonekana yapo sawa na udanganyifu
Hufunika vinywa vyao wakati wa mazungumzo
Kufunika kinywa, hasa ni hali ambayo mtu anajaribu kuzuia maneno ya udanganyifu yanayotoka kinywani kwake. Inaweza kwa kuweka mkono juu ya mdomo (kuufunga) au hata kuweka kidole katikati ya mdomo (ishara ya ssshh) hii imeweza kuonekana kutoka kwa wazazi ambao huenda wamefanya ishara hii hasa kwa watu wazima huonyesha ishara ya mtu kujizuia hisia au maneno.
Hugusa pua zao wakati wa kuzungumza
Sisi sote tunajua kuwa pua ni moja kati ya kiungo kinachopendwa kutumiwa na watu wanaozungumza uongo. Wanasayansi katika kituo cha matibabu na chakula cha kuvuta huko chicago, wamethibitisha kuwa pua ya mwanadamu hufanya kazi pale mtu anapodanganya, hutokana na kemikali zitolewazo kutokana na shinikizo la kusema uongo husababisha tishu ndani ya pua kuenea. Wakati hutoweza kuona madhara kwa haraka, kitu kinachotokea ni uvimbe. Huu unaweza kuunda hisia ambazo hutaka kugusa pua.
Huvuta kofia au kola za mashati yao wanapodanganya
Dalili nyingine za watu wanaoongea uongo huvuta kola za mashati yao na kujifanya kuwa na shughuli nyingi (busy), husababishwa na tishu za shingo na uso kutoka. Mtu anapodanganya hujenga hisia za kutazama maeneo haya ambayo muongo huyagusa gusa, shinikizo la uongo pia husababisha jasho kutoka karibu na shingo ambayo ndio sababu ya kola kuvutwa kama inavyojulikana.
Huepusha macho yao kukutazama
Hii ni katika utoto pia. Bado watu wazima tutagusa maeneo ya jicho wakati hatutaki kuangalia kitu, ni utaritibu wa ubongo kukabiliana na kuzuia udanganyifu na shinikizo la kukabiliana na mtu tunaemdanganya.
Vitendo ni zaidi kuliko maneno, kwa kutambua ishara hizi utakuwa na uwezekano mdogo wa kudanganywa, bila kujali jinsi wanavyokusikiliza na wakati mwingine hauitaji hata kulisikia jibu la kweli kwa sababu tayari utakua umepata kutoka katika lugha yao ya mwili. Jitayarishe kuchunguza ishara hizi na uangalie watu ambao watakudanganya.