Kama ulivyosikia kuhusiana na mechi ya Ligi Kuu nchini Ugiriki imesitishwa ghafla baada ya mmiliki wa timu moja iliyokuwa inacheza kuingia na bastola uwanjani akitaka kumfyatulia mwamuzi.
Mmiliki wa Paok, Ivan Savvidis ambaye ni mfanyabiashara mkubwa nchini Ugiriki aliingia uwanjani baada ya mwamuzi kukataa bao la timu yake akidai mfungaji, kabla aliotea
Mechi hiyo kati ya Paok Salonika dhidi ya AEK Athens ilivunjika dakika za nyongeza baada ya Paok kupata bao dakika za nyongeza lililofungwa na Ferndando Varela.
Wakati huo Paok walikuwa nyuma kwa bao 1-0 na hilo lilikuwa bao la kusawazisha. Lakini mwamuzi alisema halikuwa sahihi sababu ilikuwa ni offside.
PICHA HIZI HAPA..