huenda ukawa unajiuliza Nondo yupo wapi baada yakupatikana mkoani Iringa majuzi baada ya kudaiwa kutekwa na watu wasio Julikana .
NONDO ALETWA KWA DCI: Jeshi la Polisi mkoani Iringa limemkabidhi Mwenyekiti wa mtandao wa Vyuo Vikuu, Abdul Nondo kwa Mkuu wa Upelelezi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na chombo cha habari, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Juma Makanya jana baada ya kumpokea kijana huyo aliyedaiwa kutoweka mwanzoni mwa wiki hii, waliamua kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa kwa ajili ya kujiridhisha hali yake kama haijadhurika.
Kamanda huyo amesema, safari ya kumsafirisha mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ilianza jana usiku (Juzi tarehe 9) kwa ajili ya kuripoti kwa Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai kwa mahojiano zaidi.
Ambapo kazi rasmi ya upelelezi huenda ikaanza jumatatu Wiki ijayo