Monday

HUENDA MCHEZAJI HUYU AKATUA SIMBA

0 comments

Na George Mganga

Baada ya kuisadia Azam FC kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC jana Jumapili, Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema kuwa, mchezaji Idd Kipwagile anastahili kucheza nje ya Azam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Haji ameandika kuwa anatamani kumuona mchezaji huyu akisakata gozi nje ya Tanzania, huku akimpigia debe pengine ajiunge na wekundu hao wa Msimbazi, Simba SC.



Kipwagile ameonekana kuimarika zaidi katika kikosi cha Azam FC msimu huu kutokana na kasi ya mchango wake ndani ya timu hiyo.

Kutokana na ujumbe alioandika Haji Manara, inawezekana uongozi wa Simba ukawa kwenye mipango ya kunyatia mchezaji huyo ambaye yuko kwenye kiwango kizuri hivi sasa.Mar