Thursday

KUNAMTU KAAMBIWA SIMBA SIO SEHEMU YA STAREHE

0 comments


Mfaransa wa Simba, Pierre LEchantre ambaye ndiye bosi wa benchi la ufundi, amemuonya kiungo wake, Mohammed Ibrahim kwamba lazima ajue Simba si sehemu ya kujifurahisha.

Lechantre amemtaka kiungo huyo kuhakikisha anafanya kazi kwa juhudi na si kuifanya Simba kama sehemu ya mapumziko au kujifurahisha.

“Hapa si sehemu ya holiday, lazima ajue kuwa sisi tuko makini na lazima awe makini. Anachotaka kufanya hakitakubalika hata kidogo.

“Nashangazwa sana na anachotaka kukifanya, leo ana hiki, kesho ana lile. Sitaki hilo,” alisema.

Lechantre amesema Mo Ibrahim amekuwa mtu asiye makini na kama ataendelea na tabia hiyo atashindwa kufanya naye kazi.