Timu ya soka ya Tanzania Prisons ya jijini Mbeya imeendeleza moto wake kunako ligi kuu soka Tanzania Bara mara baada ya jioni ya Machi 11, 2018 kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wanatamtam Mtibwa Sugar.
Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Kumbukumbu ya Sokoine, Tanzania Prisons wamepata mabao yao kupitia kwa Salumu Kimenya ambaye amefunga katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza na 49 ya kipindi cha pili.
Aidha Mtibwa Sugar ambao wapo dhohofu msimu huu wakicheza michezo mitano bila ya ushindi wowote, bao lao la kufutia machozi limefungwa na Stamili Mbonde mapema katika dakika ya 32 ya kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penati.
Ushindi huo unawafanya Tanzania Prisons kufikisha alama 35 baada ya michezo 22 na kujiimarisha vyema katika nafasi ya tano baada ya wenzao Singida United ambao wapo katika nafasi ya nne kulazimishwa sare nyumbani na Ndanda FC.
Shooting 2-2 MCC
Mchezo mwingine wa raundi ya 22 iliyofanyika Jumapili, imeshuhudia Mbeya City wakipata sare ya mabao 2-2 ugenini dhidi ya wafunga buti Ruvu Shooting.
Bao la kwanza la Mbeya City katika mchezo huo ambao umefanyika katika uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani, limefungwa na Eliud Ambokile mapema kabisa katika dakika ya 13, kabla ya Frank Ikobela kufunga lingine katika dakika ya 53.
Mabao ya Ruvu Shooting katika mchezo huo yamefungwa na Hamis Mcha Viali katika dakika ya 61, kabla ya Ishala Juma kufunga bao la jioni katika dakika ya 90 kuwafanya kupata alama moja.
Matokeo hayo yanawafanya Mbeya City kufikisha alama 25 na kuendelea kukalia nafasi ya nane huku Ruvu Shooting nao wakifikisha alama 25 na kukalia nafasi ya tisa ya msimamo wa ligi kuu bara.
Majimaji 0-0 Lipuli
Majimaji wakitumia uwanja wao wa nyumbani wa Majimaji mjini Songea, wameambulia alama moja kutoka kwa Wanapaluhengo Lipuli FC baada ya kutoka sare ya 0-0 katika mchezo mwingine wa ligi kuu raundi ya 22.
Majimaji ambao ndio walikuwa wakihitaji ushindi katika mchezo huo kutokana na nafasi waliyopo kutokuwa rafiki kwao wameshindwa kufanya hivyo licha ya kukosa nafasi nyingi za wazi.
Matokeo hayo yanawafanya Majimaji kufikisha alama 16 na kuendelea kukalia nafasi ya 16 huku wakisaliwa na michezo nane, wakati Lipuli wao wamefikisha alama 27 na kukalia nafasi ya saba.
Matokeo yote raundi ya 22
FT: Tanzania Prisons 2-1 Mtibwa Sugar
FT: Singida United 0-0 Ndanda FC.
FT: Majimaji FC 0-0 Lipuli FC
FT: Ruvu Shooting 2-2 Mbeya City
19:00 Azam FC vs Mbao FC (Azam Complex, Chamazi)
Machi 12, 2018 : Young Africans Vs Stand United (Taifa, Dar)
Machi 13, 2018: Kagera Sugar vs Mwadui (Kaitaba, Kagera)