Thursday

MCHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA AFARIKI DUNIA

0 comments



Mchezaji nyota wa zamani wa Simba, Urther Mambeta amefariki dunia leo jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa Mambeta aliyeugua kwa muda mrefu amefariki leo.

Mambeta alikuwa mmoja wa wachezaji walioichezea Simba tokea ikijulikana kama Sunderland.

Simba ilibadilisha jina ikitokea kuwa Sunderland baada ya Serikali ya Tanganyika kusisitiza timu kutumia majina ya Kiswahili.

Mambeta alikuwa mmoja wa wachezaji walioanza kuichezea Simba mwanzoni kabisa na taarifa zimeeleza msiba wake utakuwa Kigamboni jijini Dar es Salaam.


Mwenyezi Mungu Amrehemu.