![]() |
Afisa Ustawi wa Jamii wilayani Ngara Musa Niyonsaba Balagondoza akiwa nyumbani kwa Babake na Anthony. |
![]() |
Mwanafunzi huyo Anthony Petro pichani kulia, wiki iliyopita alijulikana kupitia mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari ambapo anaishi maisha kuombaomba wasamaria wema baada ya baba yake Petro Magogwakutokuwa na uwezo kiuchumi wa kupata chakula cha familia.
Alisema maisha yake ni ya shida kwa familia kukosa mto wa mchana akishindia andazi moja na maji baada ya baba yao kukosa chakula na kutokuwa na uwezo kifedha wakati mwingine yeye na wadogo zake hutumia maparachichi kama mlo wa mchana au usiku.
Mazingira ya mwanafunzi huyo sio ya usalama kwani familia inaishi mbali na kijiji mpakani na nchi jirani ya Burundi nyumba yao iliyobomoka imezungukwa na msitu kwa maana ya miti ya parachichi, mifenezi na karatusi huku kwa majirani kukiwa na miti ya karibea na migrevelia.
“Tuhamishwe eneo hili na kujengewa sehemu nyingine, hapa watu wabaya wanaweza kuja na kutuua au kutuibia ila namshukuru Mungu nikishiba nikaenda shule nataka niwe mwalimi nakufundisha wengine”Alisema Anthony.
|
![]() |
Afisa Ustawi wa Jamii wilayani Ngara Musa Niyonsaba Balagondoza alipoutembelea Uongozi wa Shule anayosoma Anthony. |
![]() |
Pia alisema akipata chakula na kushiba hatakuwa na mawazo ya kwenda kuomba omba mpakani mwa nchi ya Burundi eneo la Kobero na kabanga mjini hivyo, atahuduria masomo na kuhakikisha anafuata atakachoelekezwa na walimu hatimaye atimize malengo kimaisha.
Afisa Ustawi wa Jamii wilayani Ngara Musa Niyonsaba Balagondoza, ametembelea Shule ya msingi Ngundusi kubaini mahudhurio ya Mwanafunzi Anthony na kufika kwa baba yake na kusema serikali na jamii wakiungana mtoto huyo na ndugu zake wataboreshewa maisha.
Amesema idara yake inasimamia na kulinda haki za watoto kwa mujibu wa sheria namba 21 ya mwaka 2009, hivyo anawashukuru wananchi walioibua mtoto huyo kwa kutumia mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu walioguswa wameanza kujitokeza kusaidia.
Ngara, Na Shaaban Ndyamukama
|
Created By OmTemplates | Distributed By Blogger Template