29680866_1809351125771456_581539159_o
Mtoto Anthony Petro akiwasili Ofisi za RADIO KWIZERA –NGARA Mkoani Kagera na ameiambia Redio Kwizera na Wasikilizaji wake kuwa hafurahishwi na maisha wanayoishi kwani hakuna usalama wa kutosha hivyo ni vema wakasaidiwa kutafutiwa eneo lingine kwa ajili ya usalama wao.
29634737_1809351325771436_1539729882_o
Akaunti ya mtoto Anthony Petro Magogwa.

 Jina la Account:

Petro, Niyosaba and Paphilius
 
A/C Na. 01523 46697000

 CRDB

 Jina la kwanza ni la baba wa mtoto

 Jina la pili ni la Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya
 
Jina la tatu ni la Paroko wao

Imefanyika hivyo ili kudhibiti matumizi ya fedha kwa kuwa watoto bado ni wadogo.
29748178_1809351292438106_1405445495_o
Mtoto Anthony Petro aliyetangulia akiwa na Baba Yake Mzazi, Mzee Petro Magogwa walipowasili Ofisi za Radio Kwizera mjini Ngara.

 Pamoja na Familia hiyo kutoa shukrani kwa wanaojitokeza kuwasaidia ,Afisa Ustawi wa Jamii wilayani Ngara mkoani Kagera Bw. Musa Balagondoza wakati akitoa ufafanuzi wa namna ya kumsaidia Mtoto Anthonykupitia kipindi cha Mchakato hapa Redio Kwizera ametoa wito kwa Watu wote walioko ndani na nje ya wilaya ya Ngara kufuata utaratibu wa kupita ofisi ya Ustawi wa Jamii ama Ofisi ya Mkurugenzi kabla ya kuifikia Familia ya Mzee Petro Magogwa.

Alipoulizwa kuhusu baadhi ya makundi ya watu waliojitokeza kuchangisha watu kwa ajili yaMtoto Anthony, AfisaBalagondoza amesema Halmashauri haina taarifa hivyo misaada yote inayotolewa kwa ajili ya mtoto huyo inapaswa kupitia kwenye Akaunti maalumu (A/C Na. 01523 46697000 Benki ya CRDB) iliyofunguliwa chini ya Halmashauri ya wilaya .
29634336_1809351215771447_2006293266_o
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya Watumishi wa Kituo cha Radio Kwizera ,Ngara wakimpokea Mtoto Anthony na Baba yake Mzee Petro Magogwa walipokuja kuzungumza na wasikilizaji wa Kituo hicho kupitia kipindi cha mchakato cha radio kwizera.