Jeshi la Polisi wilayani Ngara mkoani Kagera, limemkamata Mwalimu Deogratius Simon (34), kwa kosa la kumkashifu Rais Dkt John Magufuli kuwa ni dikteta na kwamba anaminya demokrasia kwa kuzuia maandamano na mikutano.
Mwalimu huyo kabila Mhaya ,akifundisha Shule ya Sekondari Nyakisasa,Tarafa ya Rulenge wilayani Ngara aliandika ujumbe wa kumkashifu Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo kati ya tarehe za mwaka 2016 -2018 kupitia ukurasa /akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa facebook iliyosajiriwa kwa jina la Deogratius Simon akitumia simu aina ya tecno y3 yenye laini ya hallotel.
Kufuatia tukio hilo,akiielimisha Wananchi kupitia Mashindano ya mpira wa miguu ya Polisi Jamii Cup 2018 yanayoendelea wilayani Ngara yenye kauli mbiu ya ‘’Kataa uhalifu,Fichua wahalifu’’, Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani humo,Bw. Abeid Maige ameonya baadhi ya watu wasiopenda amani ya nchi hii wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii wakivunja shieria kwa kuahamasisha chuki dhidi ya Serikali.
Bw.Maige amewasisitiza watanzania kuwa mitandao ya kijamii isitumike kuchochea uharifu kwa kuacha kutimia lugha ya kichochezi na kuwashawishi watu wengine kuvunja sharia bali itumike kuchochea maendeleo yao.
Mtuhumiwa amesomewa mashitaka yanayomkabili Katika Mahakama ya wilaya ya Ngara March 20, 2018 na amekana ambapo kesi hiyo itatajwa tena Ijumaa hii March 23, 2018.
|