Friday

NYOTA YAKO LEO IJUMAA: 2/3/2018.

0 comments




SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Weekend hii  kuna maneno  au ugomvi wa maneneo utakaotokea kati yako na rafiki yako au na watu wa familia yako. Mzozo huo utakuathiri sana kikazi na kibiashara. Vinginevyo tegemea kupata habari ya kupona kwa rafiki yako ambaye alikuwa anaugua.

PUNDA- ARIES (MACH 21-  APR 20)
Weekend hii jaribu sana kuwa na tahadhari, hiyo haraka yako ya kufanya mambo itakuletea hatari na matatizo sana mbele yako.Unaweza hata kupigwa na kuumizwa usipokuwa makini na mambo yako.

NG’OMBE – TAURUS  (APR21 – MAY 20)
Weekend hii jaribu kuwa muangalifu katika kujitetea kwa makosa uliyoyafanya na unapozungumza na mtu yoyote hata awe mdogo au mkubwa chunga sana matamshi yako. Kama una mawazo yako binafsi usiwalazimishe watu wakubaliane nayo. Katika mazungumzo yoyote leo jaribu kuwa mpole na uwaonyeshe watu kwamba unaweza ukatabu . ukifanya hivyo utafuzu jambo lako.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Kama ulikuwa umedhamiria kufanya safari ya karibu au mbali huu ndio wakati wako. Kama una kesi basi fahamu kwamba kesi hiyo utashinda, na kama ulikuwa na jambo lolote ambalo lilikuwa limekwama litafunguka. Unachotakiwa kufanya ili kufanikiwa ni kuwa makini katika ufuatiliaji tu.

KAA – CANCER (JUN  22 – JUL 23)
Weekend hii jihadhari sana kudanganywa, usimwamini  mtu yoyote katika jambo lolote na kama unataka kulifanya hilo jambo jaribu sana kufanya uchunguzi kabla ya kulifanya. Nyota zinaonyesha kwamba kuna dalili ya kupoteza fedha au mali, Tafadhali jihadhari sana.

SIMBA – LEO (JUL  24 – AUG 23)
Leo inaonekana utasononeka sana na roho kuuma  kutokana na vitendo vibaya utakavyofanyiwa na  marafiki zako ambao wanajifanya wanakupenda sana. Na kama una mpenzi wako kuwa macho sana maana marafiki hao wanamdangaya  ili afunge ndoa na  mpinzani wako mkubwa.

MASHUKE – VIRGO (AUG  24- SEPT 23)
Leo mpaka jumatano utapata habari nzuri kutoka kwa rafiki yako wa mbali ambayo itakufanya uache kazi yako uliyo nayo sasa. Hata hivyo mafanikio yako makubwa yatakuja baada ya wewe kufanya mabadilkiko aidha ya kikazi au kibiashara au makazi. Kama huna shughuli yoyote jaribu kuanzisha biashara yoyote utapata mafanikio.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Wiki hii kuna dalili ya kupata fedha na heshima kubwa katika jambo lako ambalo unalitarajia. Kama hujaoa utampata wa kumuoa na kama hujaolewa ndoa ipo njiani inakuja.  ndoa hiyo kwa nyote wawili mke na mume itadumu kwa muda mrefu na itakuwa na mafanikio makubwa.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Weekend hii mambo yako mengi yatafanyika kwa haraka kuliko ulivyotegemea. Utapata ahadi za ukweli na zenye mafanikio katika nyanja zote ziwe za  kifedha kimaisha na kimapenzi, vile vile utapata habari nzuri kuhusu watoto au watoto wako watakufurahisha

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 21)
Weekend hii sio nzuri sana kwako, kama ni mfanya biashara utakumbana na hasara au mikosi na biashara unayoifanya inaweza kukwama. Kama ni mkulima utapoteza mazao yako kama umeoa basi kunaweza kukatokea ugomvi na mkeo, kama ni mfanyakazi kuwa muangalifu sana ofisini na kama una mpenzi leo msionane nae mnaweza mkagombana na kuachana.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Weekend hii ni mbaya kwako jambo lolote utakalofanya hata liwe zuri vipi litakugeuka, nyota zinakushauri kuwa ahirisha mipango yako yote hasa kwa muda wa asubuhi na ikiwezekana mpaka kesho mchana.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Weekend hii yale yote uliyokuwa unayataka au uliyoyadhamiria yatakuwa. Na utakutana na marafiki wakweli na waaminifu watakaokuongoza katika njia nzuri za mafanikio ya kimaisha. Tegemea kupata habari nzuri kutoka nje ya nchi.