Sunday

SIKU YA SIMBA KWENDA MISRI HII HAPA

0 comments
Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka Jumatano ya wiki ijayo kwenda nchini Misri kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano wa kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry ya Misry.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumamosi ya wiki ijayo ya March 17-2018.

Kikosi hicho kinaendelea kujifua kikamilifu kwenye uwanja wa Boko Veterani Jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo huo.

Katika mchezo wa marudiano Simba inahitaji ushindi wowote ili kuweza kusonga mbele, au sare ya mabao 3-3.

Endapo Simba atapata sare tofauti na ya mabao 3-3 mchezo huo utaweza kuongezewa dakika 30 na kama matokeo yatakuwa hayo basi utaenda kwenye hatua ya mikwaju ya penalti.

Sare ya mabao 3-3 itaisaidia Simba kusonga mbele katika hatua inayofuata kwa kigezo cha kufunga mabao mengi ugenini.