Mbeya. Mamlaka ya Udhibiti wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, imepiga marufuku watu wanaohubiri kwenye mabasi ya abiria
yanayokwenda wilayani na mikoani.
Meneja wa Sumatra Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Denis Daudi ameyasema
hayo leo Machi 19 wakati akizungumza na chombo cha Havarti kuhusiana na malalamiko ya abiria kutokana na kero wanayokumbana nayo wakiwa safarini.Daudi amesema amekuwa akipokea malalamiko hayo na kwamba awali walitoa elimu kwa madereva na makondakta kutowapa nafasi za kueneza injili na ufanyabiashara, jambo ambalo halijatekelezeka.
"Nimepokea malalamiko kutoka kwa abiria na kama mamlaka  tulitoa elimu kwa waumini, wafanyabiashara hususan madereva na makondakta sasa kama elimu hiyo wanaipuuza basi tutakaowabaini tutawawajibisha," amesema.
Amewataka wanaojitambulisha kuwa ni wachungaji na kueneza neno la Mungu kwenye vyombo vya usafiri wa umma, kutofanya hivyo badala yake watumie
njia mbadala.