Kusinyaa kwa ini husababishwa na magonjwa mbalimbali ya ini kama Michomo kwenye ini inayoweza kuletwa na maambukizi ya virusi vya hepatitis B na C na unywaji wa pombe wa kupindukia. Ini hufanya kazi mbalimbali mwilini ikiwa kuondoa sumu mwilini na kemikali hatari, kusafisha mwili na kuunda virutubisho vya masingi.

Makovu na Kusinyaa  kwa ini hutokea kama madhara ya majeraha kwenye tishu za ini. Mara ini linapojeruhiwa, hujaribu kujirudisha kwenye hali ya kawaida sehemu iliyojeruhiwa, kufanya hivi makovu hutengenezwa. Jinsi makovu yanavyoendelea kutokea husababisha ini kusinyaa na hutengeneza makovu makubwa na kufanya ini lishindwe kufanya kazi zake.

Kufeli kwa ini  kutokana na kusinyaa huweza kusababsha dalili Fulani ambazo hutokea, na kufeli kwa ini ni hatua ya mwisho inayotishia uhai wa mtu.

Uharibifu wa ini unaoelekea kusinyaa  hauwezi kutibika au kuondolewa. Lakini kama ugonjwa ukigunduliwa mapema na kisababishi kimejulikana, uharibifu zaidi huweza kuzuiwa na sio kuondolewa kabisa kama ushafanyika.

Dalili

Kusinyaa kwa ini mara nyingi huwa hakuna dalili mwanzoni mpaka ini liwe limeharibika kwa kiwango kikubwa. Kama dalili zikitokea huwa ni

  • Kuchoka
  • Kutokwa na damu kirahisi(unapopiga mswaki au unapojikwaruza kidogo)
  • Kuwashwa ngozi
  • Manjano kwenye ngozi na macho
  • Mwili kutuwama maji kama tumboni na miguuni
  • Kukosa hamu ya kula
  • Kichefuchefu
  • Kuvimba miguu
  • Kupungua uzito
  • Kuchanganyikiwa, kulegea na kuongea kama mtu aliyelewa(dalili za ubongo kuharibika)
  • Wekundu kwenye viganja na mikono
  • Korodani kupungua ukubwa
  • Kukua kwa matiti kwa mwanaume

 Mwone daktari kama unafkili una dalili za kusinyaa kwa ini kwa uchunguzi na vipimo

Visababishi

Magonjwa mengi na hali huweza kusababisha tatizo la makovu na kusinyaa kwa ini.

Visababishi vya mara kwa mara ni;
  • Matumizi sugu ya pombe
  • Maambukizi/ michomo sugu ya ini inayosababishwa na virusi aina ya  Hepatitis Bna C

Sababu zingine ni kama;

  • Kujikusanya kwa madini chuma mwilini(hemochromatosis)
  • Ugonjwa wa cystic fibrosis
  • Kujikusanya kwa madini ya shaba mwilini(ugonjwa wa wilson’s)
  • Matatizo ya kiuumbaji wa mirija ya nyongo
  • Tatizo la kurithi la udhaifu wa uchakatuzi wa sukari katika seli kama(galactosemia au ugonjwa wa kuhifadhi glycogen)
  • Matatizo ya umeng’enyaji wa chakula ya kuzaliwa nayo
  • Kuharibika kwa mfumo wa nyongo(primary biliary cirrhosis)
  • Kuganda na kusinyaa kwa mifumo ya upitishaji nyongo(primary sclerosing cholangitis
  • Maambukizi kama kichocho
  • Madawa kama methotrexate

Madhara

Madhara ya kusinyaa kwa ini huwa haya;

Madhara yatokanayo na kuzunguka kwa damu

Shinikizo la juu kwenye ini- kusinyaa kwa ini husababisha mzunguko wa damu wa ini kupungua, na hivyo kuongezeka kwa mgandamizo kwenye mishipa ya veini inayotoa damu kutoka kwenye matumbo kwenye na bandama.

Kuvimba kwa miguu na tumbo- shinikizo la damu la juu kwenye ini husababisha kuvia kwa maji kwenye miguu na ini. Kuvimbakwa miguu na kujaa kwa maji kwenye tumbo kwa wagonjwa hawa wa kusinyaa kwa ini huweza kusababishwa na tatizo la ini kushindwa kuzalisha aina Fulani ya protini iitwayo albumin.

Kuvimba kwa bandama- shinikizo la damu la ini huweza kusababisha kuvimba kwa bandama. Kupungua kwa chembe nyeupe za damu na chembe mgandisho-platelets kwenye damu huwa dalili ya kusinyaa kwa ini na shinikizo la damu la juu kwenye ini.

Kutokwa damu- shinikizo la juu la damu kwenye ini huweza kusababisha damu kutafuta njia zingine na kupitia mishipa midogomidogo, na hivyo mishipa hii huongezeka ukubwa na kuvimba. Endapo itapewa shinikizo zaidi mishipa hii hupauka na kusababisha kutokwa na damu sana. Hatari ya kupoteza maisha hutokea endapo kuvimba kumetokea sehemu ya chini ya umio au tumbo maana huchangia utokaji wa damu unaoendelea. Maambukizi ya bakteria hutokea kutokana na kutokwana damu pia

Madhara mengine

Maambukizi-kama una tatizo la kusinyaa kwa ini, mwili wako unakosa nguvu ya kupambana na maambukizi. Maji kwenye tumbo huweza kupelekea maambukizi mabaya ya kuta za tumbo

Utapiamlo- kusinyaa kwa ini huweza kusababisha tatizo la mwili kumeng’enya na kuchakatua chakula na virutubisho, hupelekea udhaifu wa mwili na kupoteza uzito

Kujikusanya kwa sumu kwenye ubongo- kama ini likiwa limeharibika, uchujaji wa sumu huwa si rahisi hivyo hujikusanya kwenye mwili ikiwemo kwenye ubongo na kusabaisha kuchanganyikiwa na kushindwa kutulia kimawazo. Tatizo hili linaweza kuwa na dalili za uchovu tu au dalili zingine kali kama kutojitambua, nusu kifo au kifo kabisa.

Manjano- manjano hutokea pale ambapo ini lililosinyaa limeshindwa kuondoa kemikali za bilirubin na hivyo hujikusanya katika damu. Manjano hutokea kwenye ngozi na macho, mtu anaweza kuwa na choo mpauko au mkojo mweusi.

Magonjwa ya mifupa- baadhi ya watu walio na ugonjwa wa ini kusinyaa huwa kwenye hatari ya kuvunjika mifupa kutokana na mifupa kukosa nguvu.

Kuongezeka hatari ya saratani ya ini- nambari kubwa ya watu walio na tatizo la saratani ya ini maini yao huwa yamesinyaa pia.
Kufeli ghafla kwa ini kutokana na ugonjwa sugu wa ini- baadhi ya watu hufeli organi nyingi kwa wakati mmoja

Vipimo na utambuzi

Watu wenye hatua za awali za kusinyaa kwa ini mara nyingi huwa hawaonyeshi dalili au viashiria, kwa mara ya kwanza kusinyaa kwa ini kunaweza kutambuliwa kutokana na vipimo vya kila siku kwa mtu aliye na tabia ya kupima mara kwa mara. Daktari wako anaweza kukuagiza ufanye vipimo vya kimaabara ili kuona kama kuna tatizo kwenye ini kama kusinyaa kwa ini.

Vipimo vya maabara

Utendaji kazi wa ini- Damu itachukuliwa kwenye mishipa yako ya damu na kuwekwa kwenye kichupa kasha kupelekwa maabara na kupimwa kemikali za birilubin inayotokana na uvunjwaji wa chembe nyekundu za damu, na vimengenya vya ini kama ASAT,ALAT n.k
Utendaji kazi wa figo- Figo itatazamwa kama inatenda kazi vizuri kwa kupima kiwango cha usafishaji wa kemikali ya creatinine. Kama kukiwa na kiwango kikubwa katika damu maana yake figo haifanyi kazi vema na hili huweza kutokea kutokana na ini kusinyaa na kushindwa kufanya kazi.
Kipimo cha Hepatitis B na C- Huweza kumsaidia daktari kujua ni nini kilichosababisha kusinyaa kwa ini na kama unamaambukizi hayo.
Kuganda kwa damu- kipimo cha INR hufanyaika ili kuweza kujua uwezo wa damu yako kuganda. Ini linapokuwa linashindwa kufanya kazi uwezo wa damu kuganda hupungua na mgonjwa anaweza kutokwa na damu kirahisi na kufa. Tatizoo hili linapogunduliwa hutibiwa

Vipimovingine

Vipimo vya mionzi kama ile ya CT scan, MRI huweza kufanyika kuangalia ukubwa wa tatizo na umbo la ini, pia huweza kusaidia kutambua matatizo mengine ambata.

Kipimo cha kinyama- nyama ndogo hutolewa kwenye ini ili kupimwa maabara ila si lazima kifanyike. Daktari anaweza kutumia majibu hayo ili kutambua ukubwa wa tatizo la kusinyaa kwa ini.

Kama ukigunduliwa na tatizo la ini basi daktari wako atakushauri kumtembelea ofsini kila baada ya muda Fulani kwa ajiri ya kufanya vipimo vya uchunguzi ili kutambua ukubwa wa tatizo lako na madhara yanayoweza kuwa yanajitokeza kama vile kuvimbakwa mishipa ya damu kwenye umio na saratani ya ini.

Madhara

Madhara ya kusinyaa kwa ini huwa haya;

Madhara yatokanayo na kuzunguka kwa damu

Shinikizo la juu kwenye ini- kusinyaa kwa ini husababisha mzunguko wa damu wa ini kupungua, na hivyo kuongezeka kwa mgandamizo kwenye mishipa ya veini inayotoa damu kutoka kwenye matumbo kwenye na bandama.

Kuvimba kwa miguu na tumbo- shinikizo la damu la juu kwenye ini husababisha kuvia kwa maji kwenye miguu na ini. Kuvimbakwa miguu na kujaa kwa maji kwenye tumbo kwa wagonjwa hawa wa kusinyaa kwa ini huweza kusababishwa na tatizo la ini kushindwa kuzalisha aina Fulani ya protini iitwayo albumin.

Kuvimba kwa bandama- shinikizo la damu la ini huweza kusababisha kuvimba kwa bandama. Kupungua kwa chembe nyeupe za damu na chembe mgandisho-platelets kwenye damu huwa dalili ya kusinyaa kwa ini na shinikizo la damu la juu kwenye ini.

Kutokwa damu- shinikizo la juu la damu kwenye ini huweza kusababisha damu kutafuta njia zingine na kupitia mishipa midogomidogo, na hivyo mishipa hii huongezeka ukubwa na kuvimba. Endapo itapewa shinikizo zaidi mishipa hii hupauka na kusababisha kutokwa na damu sana. Hatari ya kupoteza maisha hutokea endapo kuvimba kumetokea sehemu ya chini ya umio au tumbo maana huchangia utokaji wa damu unaoendelea. Maambukizi ya bakteria hutokea kutokana na kutokwana damu pia

Madhara mengine

Maambukizi-kama una tatizo la kusinyaa kwa ini, mwili wako unakosa nguvu ya kupambana na maambukizi. Maji kwenye tumbo huweza kupelekea maambukizi mabaya ya kuta za tumbo

Utapiamlo- kusinyaa kwa ini huweza kusababisha tatizo la mwili kumeng’enya na kuchakatua chakula na virutubisho, hupelekea udhaifu wa mwili na kupoteza uzito

Kujikusanya kwa sumu kwenye ubongo- kama ini likiwa limeharibika, uchujaji wa sumu huwa si rahisi hivyo hujikusanya kwenye mwili ikiwemo kwenye ubongo na kusabaisha kuchanganyikiwa na kushindwa kutulia kimawazo. Tatizo hili linaweza kuwa na dalili za uchovu tu au dalili zingine kali kama kutojitambua, nusu kifo au kifo kabisa.

Manjano- manjano hutokea pale ambapo ini lililosinyaa limeshindwa kuondoa kemikali za bilirubin na hivyo hujikusanya katika damu. Manjano hutokea kwenye ngozi na macho, mtu anaweza kuwa na choo mpauko au mkojo mweusi.

Magonjwa ya mifupa- baadhi ya watu walio na ugonjwa wa ini kusinyaa huwa kwenye hatari ya kuvunjika mifupa kutokana na mifupa kukosa nguvu.

Kuongezeka hatari ya saratani ya ini- nambari kubwa ya watu walio na tatizo la saratani ya ini maini yao huwa yamesinyaa pia.
Kufeli ghafla kwa ini kutokana na ugonjwa sugu wa ini- baadhi ya watu hufeli organi nyingi kwa wakati mmoja

 TATIZO HILI LINATIBIKA HOSPITALI ENDAPO UTAWAHI MAPEMA,HIVYO BASI UONAPO DALILI ZA TATIZO HILI  WAHI HOSPITALI KUPATIWA MATIBABU