Dk. Siliacus Mutabuzi Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Akitoa Salaam za Shirika Hilo Katika Kikao.
Naye Dk.Siliacus MtabuziMwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) akitoa salaam za Shirika hilo aliupongeza Mkoa wa Kagera kwa kufanya vizuri katika chanjo mbalimbali na kusema kuwa ni matarajio yake kuwa katika Chanjo hii mpya ya Kizazi cha Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 24 Mkoa wa Kagera utafanya vizuri zaidi kwa kuwafikia walengwa wote.
Katika hatua nyingine Dk. Mtabuzi alisema kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) kama mdau Mkuu wa Afya litaendelea kushirikiana kwa karibu sana na Mkoa wa Kagera ili kuhakikisha lengo la mkoa linafikiwa na wasichana wenye umri wa miaka 14 ambao ni akinamama wa kesho wasidhurike na Saratani ya Mlango wa Kizazi.
|
Wakuu wa Wilaya Wakiendelea na KiKao Katika Ukumbi.
Mganaga Mkuu wa Mkoa wa Kagera ,Dk. Thomas Rutachunzibwa alifafanua namna chanjo hiyo itakvyotolewa katika Mkoa wa Kagera kwa kusema kuwa chanjo itaanza kutolewa tarehe 23 Aprili, 2018 na lengo likiwa ni kuwafikia wasichana 35,917 waliotimiza miaka 14 ambao walizaliwa kipindi cha Januari hadi Aprili 2004 na baada ya hapo zoezi litakuwa endelevu kwa wasichana watakaokuwa wanatimiza miaka 14 kila mwezi watakuwa wanapewa chanjo hiyo.
|
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawilo (Aliyesimama Kushoto) Aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Akisoma Hotuba ya Mkuu wa Mkoa.
DALILI ZA UGONJWA WA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI NI:-
> kuishiwa damu.
> figo kushindwa kufanya kazi.
> kuvimba miguu.
> kutokwa na usaha wa rangi ya kahawia katika sehemu za siri za mwanamke.
VISABABISHI VYA UGONJWA HUO NI:-
> kuanza mapenzi katika umri mdogo
> kuwa na wapenzi wengi
> na kuvuta sigara.
ILI KUJIKINGA NA UGONJWA WA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI NI:-
> muhimu sana wasichana wakazingatia kutojihusisha na visababishi vilivyotajwa hapao juu.
Katika Mkoa wa Kagera kuna vituo vipatavyo 56 vinavyohusika na Uchunguzi wa awali wa Ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi ambapo mkoa unatoa wito kwaakina mama kuwahi mapema katika vituo hivyo pale wanapohisi dalili hizo ili kufanyiwa uchunguzi mapema.
Kikao cha wadau wa chanjo Mkoani Kagera kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Aprili 18, 2018 kiliwahusisha:-
Wakuu wa Wilaya
Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya
Waganga Wakuu wa Wilaya
Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri
Maafisa Elimu wa Wilaya
Wadau wa Maendeleo wa Afya wa Mkoa wa Kagera
Wataalamu mbalimbali kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na na Wataalamu wa Afya kutoka katika Halmashauri za Wilaya.
|
Created By OmTemplates | Distributed By Blogger Template