Thursday

AINA ZA PLASTIC NA USALAMA WAKE KATIKA AFYA.

0 comments



Na DR JOHANES TINGA,  
MASSHELE BLOG

Mara nyingi tumekua tukitumia vifaa mbali mbali vya plastic,kutumia maji yaliyohifadhiwa kwenye chupa za plastic, kuhifadhi vyakula vya moto kwenye mifuko ya plastic. Lakini hatujawahi kufikilia kuangalia ni aina gani ya plastic je ni salama kwa afya au ina madhara kwenye afya yako. Wengi tunakumbuka kuangalia maelekezo ya vinywaji mfano maji ya chupa ila hatujali kuangalia pia ni aina gani ya plastic iliyotunza hayo maji. 
Tume

Leo katika makala hii tutaangalia aina za plastic na zipi ni salama na zipi ni hatari kwa afya ya mtumiaje.

Aina za plastiki zinaonrshwa kwa kitu kinachojulikana kama resin identification code. Yaani katika kila plastic unakuta alama ya pembe tatu yenye namba kati ya moja hadi 7 au maneno PETE,HDPE,PVC nk katikati ya alama hiyo ya pembetatu. Alama hii ndiyo inakujulisha ni aina gani ya plastic iliyotumika. mara nyingi inakua chini kwenye kitako cha chupa au kifungashio Inaonekana kama hivi kwenye chupa


Katika makala hii tutaangalia hizi aina 1 mpaka 7 ni nini hasa.
Ila kwa ufupi unashauriwa kuepuka plastiki aina ya namba 3,7 na 6. Wakati huo aina namba 1,2,4 na 5 ni salama japo zinahitaji uangalifu unapowekea kitu cha moto au kupigwa na jua kama tutavyoona mbele.


AINA ZA PLASTIKI

1. PET au PETE
hii kwa kirefu ni polyethylene terephthalate.aina hii ya plastic inatumika kwenye kufungashia vitu kama vinywaji mfano soda,maji,juisi, jam,makopo ya peanut butter,sabuni za maji nk.


USALAMA: aina hii ya plastiki ni salama kutumia japo  zinapokaa muda mrefu zinaachia kwenye kitu kilichotunzwa ndani yake  kemikali inayojulikana kama ANTIMONY TRIOXIDE. Mtu anapokula kemikali.hii kwa kiasi kikubwa inapelekea aina mbali.mbali za saratani ikiwemo saratani ya mapafu,utumbo.
Pia plastiki hii inaachia kemikali ya phthalate ambayo inaharibu mpangilio wa hormone.
USHAURI: vyema kimiminika au chakula kilicho kwenye aina hii ya plastic kitumiwe mapema kisakae muda mrefu.na ukishaitumia mara moja usitumie tena.


2.HDPE
Hii kwa kirefu ni High density polyethylene. Aina hii ya plastiki unaweza kuikuta kwenye mifuko ya plastiki, chupa za maji,soda,maziwa na juice,chupa za shampoo nk.


Hii pia ipo kwenye kundi la plastiki ambazo ni salama ila inapopata joto huachia kemikali aina ya nonylphenol ambayo inavuruga mpangilio wa hormone, inaongeza uzalishwaji wa hormone ya estrogen hata kwa wanaume kitu kinachopelekea kupunguza uzalishwaji wa mbegu za kiume na kupunguza hormone ya testosterone. Yaani kitaalamu ina estrogenic effect.

Ushauri: Pia aina hii ya plastic inaathiriwa sana na jua, inapopigwa na mwanga wa jua au kupata joto inaongeza kasi ya kuachia kemikali hizi hatari kwa afya hivyo epuka kuwekea vitu vya moto,kutunza sehemu zenye joto au kuiweka kwenye jua ( direct sunlight). Epuka kubeba vyakula kwenye mifuko ya plastiki.


3.PVC
Kwa kirefu polyvinyl chloride. Hii ni aina ya plastiki hatari sana. Inatumika kwenye mabomba nk.


Aina hii ni hatari sana kwani inaachia kemikali ambazo hi hatari kwa afya ambazo husababisha saratani na matatizo kwenye vinasaba mfano wa kemikali hizi ni bisphenol, phalates, madini ya risasi, zebaki ( mercury) na cadmium.
Na ikichomwa moto moshi wake unakua na kemikali ya vinyl chrolide ambayo inasababisha saratani ya mapafu.

4.LDPE
Low density polyethylene, hii sana sana hutumika kwenye mifuko ya plastic,vyombo vya plastiki,mifuko ya mikate na vyakula vingine vya kusindikwa.


Aina hii ya plastiki ni salama ila inapopata joto kali na mwanga wa jua zinaachia kemikali ya nonylphenol ambayo inavuruga hormone hasa hormone ya estrogen,TESTOSTERONE na kupunguza uzalishwaji wa mbegu za kiume.

Epuka kuwekea chakula cha moto, au kuweka kwenye jua wakati ikiwa na chakula.

5.PP
Hii ni polypropylene ambayo hutumika.kwenye chupa.za tomato sauce,ketchup,blueband,jibini,mirija ya kunywea juisi  nk.


Hizi ndio aina ya plastiki ambazo haziachii kemikali hatari hata ikipigwa na jua joto kali au kukaa muda mrefu.

6.PS
hii ni polystyrene ambayo.sana sana hutumika kwenye chupa au makopo ya vyakula mbali mbali.


Aina hii ya plastic inaachia kemikali hatari inayojulikana kama styrene ambayo.huweza kusababisha saratani mbali mbali na kusababisha matatizo kwenye ubongo na mishipa ya fahamu. Pia kekikali hii inapatikana kwenye moshi wa sigara na moshi wa magari.

7.Other / polycarbonate (PC)
Hii hutengeneza baadhi ya chupa za watoto.
Hii pia inaachia bisphenol ambayo.ni hatari,chaanzo cha saratani.




Bila shaka umeona umuhimu uliopo wa wewe kuangalia ni aina gani ya plastiki unayotumia na taadhari gani uchukue ili usipate madhara ya kiafya.


Unaweza kudownload makala hii katika mfumo wa PDF kwa kubofya hapa... AINA ZA PLASTIKI

No comments:

Post a Comment