Nahodha wa Simba, John Bocco amesema kuwa, wana kazi kubwa ya kufanya ili kuibuka na ushindi katika mchezo wa leo Jumamosi dhidi ya Nkana FC kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika lakini lazima washinde.
Simba itacheza na Nkana ukiwa ni mchezo wa kwanza utakaochezwa nchini Zambia wa Hatua ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba ambayo iliondoka Jumatano ya wiki hii kwenda kucheza mchezo huo, inaisaka nafasi ya kutinga makundi ya michuano hiyo mikubwa Afrika kwa ngazi ya klabu.
“Tuna kazi kubwa ya kufanya mbele ya Nkana ili tuweze kuvuka hatua hii ambayo kila mmoja wetu hapa anatamani kuona tunatinga makundi.
“Suala la kwanza hapa ni kushinda na si kitu kingine, hatufikirii matokeo mengine tofauti, tunataka kufikia malengo yetu na ndiyo maana tunahitaji kushinda,” alisema Bocco.
Ikumbukwe kuwa, baada ya mchezo huo, timu hizo zinatarajiwa kurudiana Desemba 23, mwaka huu jijini Dar ambapo mshindi wa jumla atacheza hatua ya Makundi. Atakayefungwa, ataenda kucheza mechi za mtoano kuwania kucheza hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika