Tuesday

SIMBA KUMALIZANA NA NYOTA HUYU WA NKANA KUZIBA PENGO LA OKWI

0 comments

Ili kuziba pengo la Emmanuel Okwi, tetesi zilizo chini ya kapeti zinasema kuna uwezekano mabingwa watetezi wa ligi kuu bara, Simba kumsajili kiungo mshambuliaji matata wa Nkaa Red Devils, Walter Bwalya.

Bwalya ambaye aliwapa wakati mgumu Simba haswa mabeki wake katika mechi mbili walizokutana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, ananukia kutua Msimbazi ili kuchukua nafasi ya Okwi ambaye anatajwa kusajiliwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Tayari taarifa za Okwi kuondoka Simba kwa mujibu wa mtandao wa Kawowo Sports wa Uganda, zinasema mchezaji huyo ameshamalizana na timu hiyo.

Kuondoka kwa Okwi kutawafanya mabosi wa Simba kuanza kugharamika na Nkana juu ya usajili wa Bwalya kwa kutegemeana na mkataba wake ulivyo.

Simba hivi sasa ipo katika maandalizi ya mechi mbalimbali za Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika, SportPesa Super Cup, Kombe la FA na Mapinduzi CUP huko Zanzibar.