Fasihi simulizi ina mchango mkubwa sana katika fasihi Andishi kifani n kimaudhui
A.Kimaudhui,Dhamira nyingi ambazo ndicho kiini cha maandishi mengi katika Fasihi Andishi zilikwishajadiliwa katika fasihi simulizi.Dhamira hizo ni kama vile Mapenzi,Siasa,Matabaka,Uhuru,Ukombozi,Usawa,Unyonge wa mwanamke,Uchawi na Ushirikina n.k Fasihi simulizi haijavumbua dhamira mpya kabisa bali maudhui/dhamira zote za kale.
B. Kifani,Vipengele mbalimbali vya fani ya fasihi simulizi katika kufikisha ujumbe kwa jamii zao.Vipengele hivyo ni;
1. Muundo,Fasihi simulizi muundo wake ni wa moja kwa moja pia kuna baadhi ya waandishi wa Fasihi Andishi ambao wametumia muundo wa moja kwa moja.Mfano Riwaya ya Kuli (1979) ya Shafi A. Shafi Ametumia muundo wa moja kwa moja.
2. Mtindo,Fasihi simulizi hutumia mtindo wa masimulizi pia kuna baadhi ya waandishi wa Fasihi Andishi hutumia mtindo wa masimulizi.Mfano Riwaya ya Shida (1975) ya Balisdya
3. Wahusika,Waandishi wa Fasihi andishi hutumia wahusika wasio binadamu katika kazi zao ambao kwa kawaida hupatikana katika fasihi simulizi tu.Mfano Mashetani (1971),Pambo (1975),Adili na Nduguze (1952) Kusadikika (1951) na Kufikirika (1967) wametumia wahusika mashetani ambao hupatikana katika fasihi simulizi tu. Wahusika kama wanyama,majini,mazimwi hupatikana katika fasihi simulizi tu.
4. Matumizi ya hadithi ndani ya hadithi,hapa wahusika husimulia hadithi mbali mbali katika fasihi andishi .Hawa husimuliana hadithi za kimapokeo ambapo hadithi ni kipera cha fasihi simulizi.Mfano Njozi iliyopotea (1980),Lina Ubani (1984), Mashetani (1971)
5 . Matumizi ya mtambaji hasa katika tamthiliya,Waandishi wengi wa tamthiliya wametumia mbinu ya utambaji ambapo wanakuwa na mtambaji anayetamba hadithi fulani.Mfano, Lina Ubani (1984),Nguzo mama (1980),Pambo (1975)
6.Matumizi ya mianzo ya hadithi za Fasihi simulizi,Mfano tamthiliya ya Jogoo kijijini na ngao ya jadi(1970) Kilio Chetu (1995) ,Kivuli kinaishi (1990),Riwaya hizi zimetumia mianzo maalum ya fasihi simulizi mfano paukwa……,pakawa.
7. Matumizi ya Semi mbali mbali,Fasihi andishi hutumia semi mbalimbali ambazo ni ni tanzu za fasihi simulizi.Semi ambazo hutumiwa sana ni misemo,nahau,methali,tamathali ,vitendawili na tanzu nyingine
8. Matumizi ya Ushauri na nyimbo,Waandishi wengi hutumia sana nyimbo katika kazi zao ili kuzipa mvuto,mfano Riwaya ya Njozi iliyopotea (1980),tamthiliya ya Kilio chetu wametumia sana nyimbo katika kufikisha ujumbe kwa jamii husika.