Saturday

RASMI NONDO ARUHUSIWA KUENDELEA NA MASOMO UDSM

0 comments




Mwanafunzi Abdul Nondo amerejeshwa masomoni katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) baada ya kusimamishwa masomo March 26, 2018, kusubiria uamuzi wa kesi ya jinai iliyokuwa inamkabili.



Utakumbuka  Novemba 5, 2018, Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa ilimuachia huru Nondo baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha makosa ya mshitakiwa.

Katika kesi hiyo ambayo Nondo alikuwa akikabiliwa na makosa mawili ya kudanganya kutekwa na kutoa taarifa za uongo, mahakama hiyo imemkuta hana hatia baada ya baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kueleza mshitakiwa alifikaje Mafinga.

No comments:

Post a Comment