Sunday

BAADA YA VICHAPO VIZITO: Hivi Ndivyo Simba Inavyotinga Robo Fainali ya CAF Kibabe Kama Masihara

0 comments



UMESHTUKA?…..Tulia nikuambie, wazungu walishasema Numbers Don’t Lie (namba hazidanganyi), zitaanzaje kuwadanganya Simba?, wamemkosea nini Mungu, waacheni waende Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu, zali lao hili.
Achana na kipigo cha aibu walichokipata Wekundu hao wa Msimbazi usiku wa Jumamosi cha mabao 5-0 toka kwa miamba ya Misri, Al Ahly hiyo ikiwa ni wiki mbili tu tangu wapigwe 5-0 na AS Vita, habari ya mjini ni sare ya mabao mawili waliyolazimishwa Vita nyumbani kwao dhidi ya ‘Vibonde’ wa Simba, JS Saoura.
Kwani nani alikuwa na matumaini ya Simba kuibamiza Ahly kule Misri?, hakuna bwana, kama kuna mtu ulimsikia anazungumza hivyo basi muulize kabila lake halafu linganisha na la kwako, utagundua ni mtani wenu huyo, hakuwa ‘serious’.
Wakongo leo wamejiweka mahali pagumu ambapo wasipokuwa makini wanaweza kushindwa kujiondoa. Wamejiingiza katika shimo linalotoa mwaya pekee wa wao kumaliza mechi zote wakiwa na pointi saba tu, si zaidi ya hapo.
Habari ipo hivi, Vita wenye pointi nne sasa wanajiandaa kuwafuata Saoura ambao wapo vizuri kisaikolojia baada ya kuchukua pointi moja pale Kinshasa, kwa hesabu za haraka hawa jamaa zetu wanakwenda kuacha pointi tatu kule kwenye nchi ya Waarabu. Baada ya hapo watarejea nyumbani kuwasubiri Al Ahly, kwenye hesabu zangu mimi nawapa ushindi Vita, hivyo watafikisha alama saba.

No comments:

Post a Comment