Mdude Nyagali ‘Mdude Chadema’ , ambaye ni kada maarufu wa Chadema amepatikana eneo la Inyala Mbeya Vijijini baada ya kudaiwa kutekwa na watu wasiojulikana Jumamosi jioni wiki iliyopita mjini Vwawa-Mbozi mkoani Songwe.
Taarifa za kupatikana kwa Mdude, zilitolewa na Diwani wa Kata ya Nsalala, Mbalizi, Kisman Mwangomale akisema amepigiwa simu na watu wa eneo la Makwenje Kijiji cha Inyala Mbeya vijijini, wakiomba msaada wa haraka kwenda kumbeba.