Wednesday

AINA ZA UHARIRI

0 comments



©Masshele 2019
Mwansoko 1984, anasema mhariri kazi yake kubwa ni kunyoosha lugha, kuonesha bayana makosa na kunyoosha usanifu wa sura.

Besha 2005 anataja Sina zifuatazo za uhariri

° Uhariri wa kina
°Uhariri wa jumla
°Uhariri wa kiushikamani
°Uhariri wa Martini.

Uhariri wa jumla. Huyu hushughulikia maswala yote ya kiuhariri, kuanzia kutafuta mswada, mwandishi, kuwasiliana na mwandishi, kuandaa mkataba, na kupendekeza mswada uchapishwr au LA!

Kazi zake

-Kutafuta maeneo ya kufanyia kazi
-Kutafuta mswada unaofaa kuchapishw-kuwasiliana na mwandishi
-Ndiye anayetoa maamuzi ya mwisho ikiwa mswada uchapishwe au
-Lazima abainishe manufaa ya kampuni
-Kuandaa mkataba kati ya kampuni ya uchapishaji na mwandishi.


Mhariri wa kina.
Hushughulika na maudhui na mtindo wa mswada.
-lazima atambue lugha inayofaa.
-kunyoosha maelezo
-Anabainisha na kuondoa migongano ya hoja au kupishana kwa maelezo.
-kuangalia kama mwandishi amezingatia mtindo wa kampuni.

Uhariri wa Matini.

Hushughulika na masuala ya kiufindi kama lugha, makosa ya kiuandishi, mpangilio wa Martini, vichwa vya habari n.k
-anajukumj la kuyaweka mwandishi kuwa bora
-kuhakikisha yanamfikia msomaji katika ubora unaofaa
-kupendekeza vielelezo
-kupendekeza mwonekano wa kitabu
-Kutayarisha mswada kwaajili ya kuchapishwa
-Kusoma prufu


MISINGI YA UHARIRI WA MATINI
1. Kutimiza matakwa ya watu watatu, mwandishi, kampuni, msomaji
2.Lazima ahakikishe kazi ina uwazi , ulinganifu, inaleta maana,

3. Matumizi ya ujumi , itikeli na maadili.
www.masshele.blogspot.com

No comments:

Post a Comment