Muasisi Wa elimu mitindo,
Mikabala ya elimu mitindo,
Mitazamo ya elimu mitindo.
Aldin K. Mutembei
- Dhana ya Mtindo: Ni nini?
- Mikabala mbalimbali
- Elimumitindo kama somo
- Historia ya Elimumitindo
- Mchomozo: Ni nini?
- Ukengeufu
- Usambamba
- Ukariri
Utangulizi…
- Elimumitindo ni ufafanuzi na uchambuzi wa ujitokezaji wa mitindo tofauti katika kutumia lugha.
- – Ndani ya mfumo wa lugha, yale yanayoongelewa yanaweza kuwasilishwa kwa namna tofautina kwa zaidi ya mtindo
- Wataalamu wameufafanuajeMtindo?
MAANA YA MTINDO
- Kuna namna 4 za kuangalia maana ya mtindo.
- Mtindo kama Uchaguzi ktk Lugha
- Mtindo kama ukiukaji wa taratibu za lugha;
- Mtindo kama ujirudiaji wa muundo wa kiisimu
- Mtindo kama ulinganishi
Mitazamo kadhaa ya MTINDO
- “Mtindo ni mtu mwenyewe “(Buffon)
- “Mtindo ni kina” Darbyshire
- “Mtindo ni Ukiukaji-Ukengeufu”Enkvist
- “Mtindo ni matokeo ya mafanikio ya mwandishi katika kuifanya lugha ikubaliane na mawazo ya tajriba yake (Middleton Murry)
- “Mtindo ni ukengeufu uliokatika muktadha wa Kiisimu” (Enkvist)
- Mtindo ni uchaguzi wa sifa za lugha zisizobainifu (Bloomfield)
- Mtindo ni Kisawe cha neno au Ujielezaji (Benedetto Croce)
- “Mtindo ni muundo, mfuatano, na sulubu ambazo huvuka mipaka ya sentensi moja (Archibald Hill )
- Wanachosema hawa wote tunakifupisha kuwa:
Mtindo ni Uchaguzi
- Kuna sababu nyingi za kimtindo ambazo humfanya mtumiaji kupenda umbo moja la kiisimu kuliko mengine. Sababu hizi ni za namna mbili. Zile zinazoegemea mtumiaji na zile zinazoegemea muktadha wa lugha husika.
- Sababu za Mtumiaji: Umri, Jinsia, Upendeleo binafsi, Dini, Ukanda, Mazingira ya Kijamii yaliyomkuza mtumiaji n.k.
- Muktadha: Hutokana na mazingira ya kimawasiliano, Namna ya mawasiliano – kwa sauti au maandishi, ni ushiriki ktk mazungumzo au ni mzungumzaji mmoja tu, urasmi wa mazungumzo, hisia, uwanja wa mawasiliano (ni eneo gani –maalumu, rasmi, isorasmi, kitaaluma, kimitaani, utani, sala, n.k)
Mtindo ni Ukiukaji taratibu
- Mtindo kama ukiukaji (au ukengeushi) kutoka katika kaida za lugha zilizokubaliwa ni dhana inayotumika ktk elimumtindo kuelezea kuwa lugha ya kifasihi huruhusu utofauti na uhuru wa kukiuka.
- Ktk ushairi na katika tanz nyingine za kifasihi.
- Ubadilishaji wa mitindo na maumbo ya ushairi
- Ubadilishaji wa maneno au miisho yake
- Ubadilishaji wa maana za maneno
- Ufuatanishaji wa maneno yenye maana tofauti katika sentensi: Zamani za Siku hizi (Mlama)
- Mfu atembeaye katika uhai wa kifo cha kimya N.k
Mtindo ni Ujirudiaji
- Mtindo si suala kuwa sawa kisarufi, bali utumiaji wa maneno kwa usahihi. Usahihi huu unapimwa kwa ujitokezaji. Uwe wa mara moja, mbili au zaidi.
- Usahihi unaweza kuletwa na idadi ya ujitokezaji wa umbo la kiisimu.
- Ujirudiaji husababisha kujulikana kwa maana inayokusudiwa.
- Katika muktadha wa kishairi ujirudiaji husisitiza wazo, dhana au fikra ktk maneno au mistari ya shairi.
- Ujirudiaji wa aya fulani, wa wazo fulani, wa wahusika fulani, wa safari fulani, wa misemo na tamathali mbalimbali. Yote haya huwa ni mbinu ya mtindo ili kusisitiza au kutokeza maana inayolengwa.
Mtindo ni Ulinganishi
- Mtindo kama ulinganishi huwa kama kiunzi ambacho kwacho miundo kadhaa hulinganishwa.
- Ulinganishi baina ya matini za mwandishi mmoja, baina ya waandishi wa utanzu mmoja, baina ya tanzu na waandishi wake.
- Wahakiki hulinganisha nini? Mawazo, Mfumo wa uandishi, Fikra, Hulka, Namna za kuanza kazi, Matumizi ya wahusika wanaofanana, Matumizi ya msamiati, tamathali, muundo wa maneno n.k
Mtindo hadi Elimumitindo
- Kwahiyo hatuna budi kuangalia mtindo ni nini. Mtindo ni upekee katika uandishi unaomtofautisha mwandishi mmoja kwa mwingine Au aina moja ya maandishi kwa nyingine.
- Mtindo ni matokeo ya namna mwandishi anavyofikiri kuhusu anachokiandika na namna anavyowasilisha fikra yake kwa mlengwa mahususi na muktadha maalumu
- Kwahiyo, baada ya kuangalia Mtindo je Elimumitindo ni nini?
Elimumitindo ni Nini?
- Isimu ni taaluma ya inayoiangalia lugha kisayansi, na Elimumitindo kama sehemu ya taaluma hii huangalia vipengele vya lugha vinavyoifanya iwe tofauti (David Crystal)
- Elimumitindo ni mkabala wa kiisimu katika fasihi ukielezea uhusiano wa lugha na dhima ya kisanaa ukilenga kuuliza: kwanini na kwa vipi (Geofrey Leech)
- Elimumitindo ni dhana inayotoka kwa urasimi wa Kirusi ambapo hulenga kuelezea ukiukwaji wa hali ya kawaida ya lugha (Willie Van Peer)
- Elimumitindo ni dhana inayoweka pamoja uhakiki wa kifasihi na isimu (Henry G. Widdowson)
Elimumitindo kama somo
- Ni somo la matini ya kifasihi katika hatua ya juu ambapo mchambuzi huangalia athari maalumu ziletwazo na uchaguzi au mtindo wa lugha katika kuwasilisha maana ya kifasihi (H.H. Zhang).
- Ni Sayansi inayojaribu kugundua ni kwa namna gani wasomaji huitambua lugha (hasa ya kifasihi) katika matini ili ugunduzi huo usaidie kueleza namna tunavyoelewa, na tunavyoathiriwa na matini wakati tunaposoma.
- Kwahiyo, ni tawi la Isimu linalochunguza MISINGI na MATOKEO YA UCHAGUZI na MATUMIZI ya maneno, sarufi yake, mofolojia na fonetiki na aina nyingine za vipengele vya lugha kama mbinu za uhamishaji mawazo na hisia za mwandishi katika mazingira mbalimbali ya mawasilino .
Elimumitindo Historia na Somo
- Kama sehemu ya Isimu (Sayansi ya Lugha), ilienea zaidi ktk nusu ya pili ya Karne ya 20.
- Hii ni baada ya wataalamu wafuatao kuchapisha kazi zao zilizoeleza somo hili:
- Roger Flower : Essays on Style in Language.
- Donald Freeman : Linguistics and Literary Style.
- Geoffrey Leech : A Linguistic Guide to English Poetry na
- Thomas Sebeok : Style in Language.
HISTORIA ya Elimumitindo
- Mtu ambaye hatuwezi kumsahau katika kuendeleza somo hili niRoman Jacobson. Hasa baada ya kuandika Makala aliyoiita:
- Closing statement: Linguistics and poetics
- Huu ulikuwa ni mwendelezo wamabadiliko katika uhakiki kutoka katika mkabala wa kuhakiki kazi ya kifasihi kwa kumwangalia mwandishi na sasa kuangalia kazi yenyewe, lugha yake na namna ilivyoandikwa ili kutoa ujumbe na maana. Kutoka NINI kwenda KwaVIPI
Historia- kwanini Roman Jacobson…
- Mabadiliko katika uhakiki yaliangalia zaidi athari ya matini kwa msomaji. Hata hivyo, athari hizo hazikufuata vigezo maalumu.
- Jacobson aliona haitoshi tu kuegemea katika ufahamu wa akili ya mhakiki, bali kuwapo kwa vigezo mahususi. NI KWA VIPI
- alikuwa mwenye uwezo mkubwa kitaaluma na aliunganisha mikabala (au matapo) mbalimbali ya mawazo kwa pamoja. Alikuwa na nadharia zake binafsi.
Roman Jacobson
- Akitokea Moscow (mkabala wa kimoscow), alikwenda Prague(akajiunga na mkabala wa Umuundo) . Mawazo yake yaliwaathiri sana wana Umuundo wa Prague.
- Baadaye alihamia Marekani na huko aliwaathiri Wanamkabala wa Kimarekani na kukuza Somo la Elimutindo kufuatia Nadharia na mawazo yake.
Baadhi ya Mikutano Muhimu
- Mjadala wa Kwanza ulihusu: The problems of style “Issues of linguistics” in 1954
- Mkutano 1 kuhusu Mtindo – Indiana University , Makala zikachapishwa 1960zikisimamiwa na kuhaririwa na Thomas Sebeok
- Mkutano 2 Mtindo, Moscow State Pedagogical Institute of Foreign Languages in 1969
- Kongamano , Italy: Proceedings under the editorship of Prof. Chatman in 1971.
Tofauti za Elimumitindo Kiisimu na Kifasihi
Linguistic stylistics studies functional styles of a language and the elements of language from the point of view of their ability to express and cause emotions
Literary stylistics studies expressive means and stylistic devices characteristic for a definite work of art, man of letter, literary movement, trend or epoch, and factors influencing the expressiveness of language.
DHANA YA………..
Mchomozo
Ukengeufu/Ukengeushi
Usambamba
Ukariri/ Takriri
Ukengeufu/Ukengeushi
Usambamba
Ukariri/ Takriri
Mchomozo
- Angalia Taswira hii
- Beberu ni MBAYA kuliko shetani
- Ni Dhana gani ninayotaka ibaki vichwani mwa wasomaji?
- Kutokana na Upakaji Rangi
- MCHOMOZO ndio huibadili lugha kuwa ya KIFASIHI
- Kwa mujibu wa Halliday, tunaweza kusema kuwa bila mchomozo hakuna fasihi.
- Katika matini au simulizi fulani, kinachokuvutia na ukaipenda sanaa ile, sio lugha, bali namna lugha ilivyojitokeza ikawa tofauti na lugha uliyoizoea hata ikavuta hamu ya macho yako na kuinasa hisia yako.
- Katika mazungumzo ya kawaida,LUGHA hujitokeza ili kukidhi mawasiliano ikiwa inafuata kanuni zilizowekwa na ambayo ni ya msingi
- Nje ya mazungumzo ya kawaida kuna LUGHA YA KIFASIHI. Ndani ya uga huu, lugha inaumbwa ili ivuke kaida au kanuni na kuleta mawasiliano ambayo ni zaidi ya misingi ya lugha.
- Kwa hiyo MCHOMOZO ni dhana ya Kifasihi na Kiisimu ambayo humaanisha kuwa katika lugha neno moja au zaidi, sauti, sentensi, au maana hujitokeza zaidi kuliko kawaida na hivyo huvuta usikivu tofauti na miundo mingine ya lugha.
- Mchomozo unaweza kuwa ni wa Kimofolojia (maneno), Kifonolojia (sauti), Kisintaksia (muundo wa sentensi) au Kisemantiki (maana).
Utokezaji wa Mchomozo
Ukengeufu/ Ukengeushi
- Ukengeufu hutokea pale ambapo kanuni za muundo fulani (au matarajio yetu katika mawasiliano) hukiukwa.
- Ukengeufu wa Kimsamiati
- Ukengeufu wa Kisarufi
- Ukengeufu wa Kifonolojia
- Ukengeufu wa Kiunukuzi (uandishi)
- Ukengeufu wa Kisemantiki.
- Ukengeufu wa Kilahaja n.k
- Ukiukaji huu huleta mvuto wa kipekee na hivyo hutokeza mchomozo.
Usambamba
- Usambamba ni mbinu ya kutumia vipengele vya sentensi ambavyo hufanana au hukaribiana kisarufi, katika muundo, sauti, maana au mizani (katika ushairi)
- Ni Mbinu ya Kifasihi, ambapo sehemu ya sentensi inajirudia; liwe ni neno, sauti, muundo au hata maana.
- Mbinu hii husaidia kukuza kumbukumbu na kuamsha ari ya kupenda sanaa ya lugha.
- Usambamba huweza kutokea ndani ya sentensi 1 au zaidi; katika aya, au hata sura za matini.
- Ni kutokana na mbinu hii ndipo tunapata Ujirudiaji wa muundo au ukariri.
Ukariri
- Ni aina ya tamathali ambapo ujirudiaji wa neno, sauti, sentensi, au muundo fulani, au hata maana, taswira n.k hufuata mantiki fulani na hivyo kumvutia msikilizaji au msomaji.
- Ujirudiaji huu huwa katika muundo maalumu, na nafasi maalumu, na Lengo kuu likiwa ni KUONGEZA MSISITIZO
- Kuna Ukariri wa aina mbalimbali katika lugha. Lakini sisi tutaangalia wa aina MBILI TU
- Wa Mwanzoni wa Sentensi na wa Mwishoni mwa Sentensi.
Ukariri wa Kianafora
- Anafora (Anaphora) huwapo pale ambapo NENO au MANENO hutokea MWANZONI mwa sentensi mbili au zaidizinazofuatana.
- MIFANO
- Kweli naitiya tamma, nikuage ndugu yangu
- Kweli si mwenye kukoma, kuwambiya walimwengu
- Kweli siyati kusema, katika uhai wangu
- Nami kwa upande wangu, hiyambiwa ‘takubali
- Katika ushairi (Nyimbo, Tenzi n.k)
- Hotuba inayovutia hutumia sana mbinu hii.
Ukariri wa Epifora
- Epifora (Epiphora) huwapo pale ambapo NENO au MANENO hutokea MWISHONI mwa sentensi mbili au zaidizinazofuatana.
- Mstari wa mwisho wa shairi. (mwisho wa kila ubeti)
- Kama tabu ni mauti, leo nsingekuwako
- Ningekuwa ni maiti, ‘mebakiza sikitiko
- Ningekuwako tiyati, matanga ndilo funiko
- Leo nsingekuwako, Kama tabu ni mauti