Mtoto wa Faru John anayefahamika kwa jina la Faru Rajab amezua gumzo katika mitandao ya Kijamii baada ya baadhi ya wadau kuhoji jina hilo.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya hivi karibuni ya hifadhi ya Serengeti walipongeza kazi nzuri inayofanywa na Faru Rajab kwa kusaidia kuongeza idadi ya faru katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla ameingilia kati mjadala huo na kuahidi kufuatilia sababu ya mtoto wa faru John kuitwa faru Rajab na kuongeza kuwa huenda faru Rajab alibadili dini baada ya kuoa au amefuata dini ya mama yake baada ya baba yake Faru John kufa.
Faru John alikufa Agosti Mosi mwaka jana kwa maradhi na uzee huku Tume ikiundwa kuchunguza kifo hicho kilichokuwa kichodaiwa kuwa na utata.
Faru John ndiye aliyekuwa Faru mwenye umri mkubwa zaidi na aliyekuwa na sifa ya kuzalisha na ubabe katika Hifadhi ya Serengeti nchini.

0 Comments