DONDOO
Utangulizi
Maana ya malumbano ya Watani
Maana ya majigambo
AINA ZA MALUMBANO YA WATANI NA MAJIGAMBO
TOFAUTI YA MALUMBANO YA WATANI NA MAJIGAMBO
HITIMISHO
MAREJELEO
MAANA YA MALUMBANO YA WATANI
Wanyala, S.F ( 92013). Malumbano ya watani ni maneno ya kufanyiana mzaha au dhihaka kwa kueleza mwenendo au utaratibu wa maisha ya jamii husika.
Utani huambatana na ubadilishaji wa maneno au misemo ambayo huonekana kama kero, matusi au kukashifu. Kuna utani wa aina mbalimbali kwa mfano utani wa kiukoo utani wa kikabila, utani wa kirafiki, utani wa kimaeneo, utani wa kisiasa na utani wa kiumri
. MAANA YA MAJIGAMBO
Kwa mujibu Collin, K.M na Ngamia, F.O (2004) Majigambo ni shairi la kujisifu hutungwa na kuimbwa na mhusika mwenyewe. Majigambo hutungwa kwa kutumia mbinu mbalimbali za usanii kama vile, fitiani, ishara, tafsiri, vidokezi n.k
Mwenye kujigamba hujitungia shairi lake kufutia tukio maalumu katika maisha yake kwa mfano kuingia jandoni, kuoa, kurejea kutoka vitani, kushinda jambo gumu, kama kesi mahakamani, mnyama mkali, mchezo, masomo n.k
Baadhi ya majigambo huwa marefu sana na yenye masimulizi ndani yake. Lakini mengi ni mafupi. Majigambo hueleweka kwa urahisi kwa hadhira iliyokusidiwa. Mambo yanayozungumziwa huwa hadhira inayofahamu au wamewahi kuyashuhudia. Majigambo huwasilishwa kwa kuyashuhudia. Majigambo huwasilishwa kwenye sherehe maalumu
. AINA ZA MAJIGAMBO
Pembeni, Ni tungo ambazo zimekusudiwa kusifu watu wa aina Fulani tu. Pembeni hutumiwa na watu kusifia wapenzi wao, rafiki zao, watani wao, watoto wao n.k
Tondozi, tungo za kusifu vitu, kwa mfano mti, jiwe, mlima, kijiji, nchi, ng’ombe, mbuzi, samaki, nyama pori, matokeo, baiskeli n.k
Muundo wa majigambo huzingatia
Jina la sifa mhusika au jina halisi
Sifa za nasaba yake kuumeni
Maelezo ya matendo matukufu aliyoyafanya
Ahadi za kutenda makubwa zaidi kwa ajili ya mkubwa wake (mzazi, mtawala, umma n.k)
Hitimisho kujikabidhi rasmi kwa mkubwa
Kwa asili majigambo hayaandikwi hutugwa kichwani tu kabla au wakati wa utambaji. Ila siku hizi baadhi ya watu wameanza kuyatunga (au kutungiwa) kwa kundika halafu husoma au kusomewa majigambo haya wakati wa sherehe inayohusika (kama vile arusi) Haya ni maigizo ya kisasa ambayo bila shaka yanaashiria kubadilika, kama si kufa, desturi hii ya kale.Kwa mujibu wa Wanyala, F.S (2013)
TOFAUTI YA MALUMBANO YA WATANI NA MAJIGAMBO .
TUKIANZA NA UTANI
Asili ya utani ni kitenzi kutania chenye maana ya kumfanyia mtu mzaha au stihizai
Hufanyika kwa majibizano au malumbano na huwa katika maongezi ya kawaida
Hutumia lugha ya ucheshi na chuku
Huzuka kati ya jamii au koo ambazo ziliwahi kukosana hapo awali
Mada hubadilikabadilika kwa mujibu wa wahusika na muktadha
Huburudisha wahusika na hasa wanao shuhudia malumbano haya ya utani
Mifano ya utani:-
Ukitaka kujua kama mkikuyu amefariki, gongesha mapeni, ataamka na kudai ni yake.
Waluhya waliapa ya kuwa wataacha mambo yote duniani isipokuwa wanawake, upishi, ubawabu na uchawi.
Yeye ni mrefu mpaka anauza njugu karanga kwenye ndege
Kwao ni wengi mpaka wakati wa kishuka wanatumia masijara
Yeye ni mweusi mpaka haumwi na mbu usiku
Mfano 1: Sherehe za mbina katika jamii ya wasukuma hasa mkoa wa Shinyanga katika wiliya ya Bariadi, Meatu na Shinyanga sherehe hizi huhusu malumbano ya utani ya kutambiana kati ya pande mbili ambazo ni mahasimu. Utani huu hufanywa haswa na wanawake kwa wanaume ila ila mahudhurio ni wanawake ka wanaume ambao huzunguka kundi moja hadi jingine. Watambaji ambao ni wanaume huwa wamevaa kengele miguuni na mikononi pamoja na kujifunga nguo ya kaniki. Hutambiana kwa nyimbo zifuatazo ambazo huwa ni kutoka kundi la wagalu na wagika.
Fani hii ya utani japo imepotea katika jamii nyingi, bado inaonekana kuwa na faida nyingi sana miongoni mwa jamii nyingi ambao bado wanaendeleza.
AINA ZA UTANI
KOMEDIA
Hata hivyo imeanza kujitokeza hapo na pale katika komedia na katika vyombo vya mawasiliano. Mfano – utani wa mwana – komedia Owago Njiro Ujaluo utakuua! Katika kiwango cha watoto utani unajitokeza kupitia mchongoano ambao ni marufuku sana kwa watoto kwa ajili ya maelezo haya utani unaweza kugawana katika mafungu yafuatayo:-
Utani kati ya ukoo (mbari) na ukoo
Utani kati ya jamii na ndugu
Utani kati ya kabila moja na nyingine
Uatni wa kirafiki kati ya marafiki
Utani kati ya watu wa jamii moja wanaoishi katika wilaya tofauti mfano Wakikuyu wa kiambvo na Muranga
Utani miongoni mwa jamii mbalimbali
Utani hutokea katika jamii nyingi kwa watu kufanyana stihizai au masihara bila yeyote kuudhika. Endapo jambo hilo la utani limesemwa na mtu ambaye si mtani wa jadi wa jamii husika mwenye kutaniwa hulalamika na kusema mimi siyo mtani wako hivyo tuheshimiane.
Aidha utani huu unapotokea unatekeleza dhima Fulani kama vile kukejeli, kuumbua, kuburudisha, kuchekesha, kukosoana, kujengana, kuhifadhi mila na desturi, kuadilisha, kufunza maadili, kuadibu, kutia adabu. Aidha utani hujenga uhusiano wa maelewano mazuri baina ya wale wanaotaniana.
ELIMU
Utani baina ya wazee na wajukuu wao hulenga kutoa elimu ya mwanzo kwa watoto. Mfano katika utanzu huu babu na bibi wamepewa la kutaniana na wajukuu wao ili kuwatolea elimu na kuwahamasisha kimaadili.
Wazizi wanapotoa elimu hii huwa ni kwa kukemea isiyo na upole lakini babu na bibi wanapotoa elimu hii huwa siyo kwa ukali bali kwa upole. Hawa huwatania wajukuu wao hasa kwa mambo anayoweza kuonekana kuwa ni ya aibu kwa wazazi ili kuwalainisha.
MJUKUU
Akiwa mdogo babu humtania mjukuu wake wa kike. Nimeshakwisha kukuoza na yule mwendawazimu anayezurura pale sokoni hata mahari nimekwisha pokea.
Haya yanaelezwa kumkosoa anayetaniwa kuwa haendani na maadili yanayotukuzwa na jamii ni anahitajika kujistahi kama anataka kuolewa na mume wa maana.
Sifa mojawapo ya utani ni kuwa watani hujua ni lini na kwa kiasi gani na nani wa kumtania kutegemeaana na mila na ada za jamii husika. Hii ni kwa kuwa utani una mipaka. Katika utani ni lazima watu waheshimiane na hufanywa na watu wanaoelewa lugha ya jamii yao vizuri
BIBI
Katika jamii nyingi mjukuu wa kiume wa kwanza huchukuliwa na bibi kuwa mume wake. Hii ni kwamba hupata jina toka kwa mumewe.
Mifano ya utani
Nyimbo za wagika
Nale wa wila bhanu bhiswe
Bhangalu bhalosinho
Tukalemaga manumbu
Bakasamyijaga mumingunda yabho
Tegelekagi Bhakima na bhagosha na muwite
Bhing’we bhajinja Ng’ombe
Dimagi chiza mkupandeka bhalimi
Namang’ombe amatale
Bhia kuja mubhangalu bhakalimilaga makono
Nzogwi kubhagika tubhize basabhi
tafsiri
Nawaambieni watu wetu
Wagalu ni wachawi sana
Huwa tunalima viazi
Wanahamishia mashambani mwao
Sikilizeni wanawake na wanaume niwambie
Nyie weuza ng’ombe
Chungeni vizuri mtapata ng’ombe walimao
Ng’ombe wakubwa walioshiba
Msiwafuate Wagalu wanaolima kwa mikono
Njooni kwa wagika tuwe matajiri
Mfano:- Utani wa Wahaya kwa wakuria wakati wa misiba.
Kihaya
Tweija kubalaba inywe abataina kantu, mwelizaliza mwine njala. Kutuije tubatekele obujini obugali shana enjala kelewa mlalekeka kulila. Waleba mwabulwa amahela gukugula enyama mwabanza kwita ente. Mbwenu tulebe nkelatugola.
Katugende kushenya enku tuije tubage ente yangu eyomwaita tubatekele mulye mlekele kulila enjala. Katulaluga kushenya enku tuije kubatahila amaizi mwije mwoge: kamulamala mujwalege mulekele kwelizaliza. Ente yomwaita itwe tutwikugyenda, ntuija kubabagila ezindi kuluya umuhigo, enkoko ne mbata ne mbuzi mulye mugute olwokube ienjala niyo elikubaliza.
Tafsiri
Tumekuja kuwaona msio na kitu, mnalia tu kwa sababu ya njaa zenu. Ebu tuwapikie uji na ugali labda njaa zenu zikiisha mtaacha kulia. Mmekosa hela za kununua nyama sasa mmeuzauza kuu ng’ombe. Sasa ngoja tuone kama atatutosha. Ngojeni twende tukaichanje kuni tuje tuwachinjie ng’ombe wenu mliomnunua tuwapikie mle mwache kulia njaa. Tukimaliza kutafuta kuni twende kuwachotea maji muoge na mkimaliza mvae vizuri muache kuliaalia. Ng’ombe mliyemuua sisi hatumuhitaji, tutawachinjia kwengine toka zizini, huku, bata na mbuzi mle mshibe kwa sababu njaa ndio inawaliza.
Kabila la Wakuria, wahaya hujitokeza na kuanza kuwatania na kumuita marehemu ng’ombe aliyeuwawa kwa sababu ya kukosa pesa za kununua nyama. Wao huensdelea na kuvamia zizi na vibanda vya kuku na bata na wanyama wengine walio kwenye mazingira hayo na kuwachinjia ili kuwatumia kama kitoweo kwenye msiba huo.
Mwisho wa mchakato mzima wa matenga hujitokeza uharibifu wa baadhi ya vitu. Mfano kuchinja wanyama wadogo na kukata ndizi zilizochanga ambazo haziwezi kuliwa.
MAJIGAMBO.
Wahusika huigiza kwa kutumia lugha nzito yatamathali, picha na taswira zenye hisia na mawazo mazito
Majigambo huwa na matumizi ya chuki
Husaidia kuelimisha, kuadilisha na kuhifadhi mila na kuzipokeza kwa vizazi vipya.
Majigambo hujitokeza katika sherehe mbalimbali kama tohara (khubita na khulonga katika jamii ya wabukusu), Mazishi na maonesho ya kisanaa.
Mfano 1:-
Ni mimi mtanzania
Naingia kama seti Benjamini
Aliyetembea kwa mguu
Toka Arusha hadi Dar-es salaam
Naingia mwanaume shujaa
Kama nyerere kiongozi wa Tanzania
Ni mimi niliyepiga ziwa kofi
Likatapika dagaa
Naingia mototo wa kakwei na kasenene
Mzaliwa wa kijiji cha Tanzania
Masurufu ya msafiri hayaozi
Nasema nanimpenda kutawaliwa?
Je, asiyependa ujamaa ni nani?
(Mulokozi, M.M 1996)
Mfano 2:-
Mimi ni jabali lizuialo tufani kwa kiganja
Kifua changu hata radi haipenyi
Yangu si ngozi ya kawaida
Vigumba vya mikuki huvunjika vikiigonga
Hata kimbuga hutoweka kinianapo
Hakuna ajuaye asili yangu
Hakuna awezaye kutabiri hatima yangu
Apingaye athubutu ajitokeze
Mfano 3: - Majigambo ya wajaluo
Kiikongato, jadongogi ojendegueyo kagitingo lingangla
(tonggi okumba)
Gi gweyo kama,
“Le le duto, le le duto
Makata gor”
“kata obed mokieva”
Tho okama aliya
I bed mokievatho kana aliye
I bed mokieva tho omayaatwo
Sechego jodongogi ojende otigo tonng kod okumba jomanxine suchego go nduru
Tafsiri
“Kila mnyama ni mnnyama hata nguchiro”
Hata usiponipenda kifo kimenitunza kiporo
Usiponipenda kifo kimenitunza kiporo
Usiponipenda kifo kimenianika nakauka
Majigambo haya hutokea wakati wa matanga. Wazee na vijana huwa wamebeba mikuki na ngao huku wanawake wakipiga manyowe. Suala hili la kujigamba hutokea hasa kwa watu katika jigambo hili vipengele vinavyohusu nasaba vinaachwa labla kwa kuwa havina uhusiano na muktadha wa kisiasa wajigamba hili, ila baba na mama ya mjigambaji wametajiwa (kakwezi na kasenene). Hata hivyo tamate alizinazo tumika ni za kijadi
Mtambaji anajisifu kuwa yu shujaa ‘kama Nyerere na kwamba alikaa juu ya mtini nikakojoa kwenye chupa”. Hapa anadhihirisha uwezo wake wakati miza lile alilolinuia (kama Nyerere?)
Matumizi ya maneno kama “kukojoa yanadhihirisha kuwa katika hii mjigambaji anao uhuru wa kutamka hadharani baadhi ya maneno ambayo katika mazingira ya kwaida yangefikiwa kuwa ni matusi” (Tafsiri ya Dict. Rubanza alitumia tafsiri ya kujisaidia Rubanza 1994;17)
Majigambo hutumia sitiari nzito zenye kuonyesha ushujaa na ukali. Mjigambo huweza kujiita “mkuki’ “nduli” “samba” “ng’ombe dume” ncha ya mkuki” . jigambo hili pia linatumia sitiari kwa mfano, kuna jazanda (au msemo wakisitiani) ifuatayo:-
“Ni mimi niliyepiga ziwa kofi; likatapika Dagaa, huenda ikahusiana na kupata watoto. Kwa ujumla, sitiani hii imelazimishwa tu kuingia hapa kwani si muktadha wake, Huenda mjitambaji (motto wa shule) hakuelewa maana yake.
Wenye umri mkubwa
Mfano 4:- majigambo ya Waha
Majigambo katika jamii ya Waha hususani katika sherehe za kulipa mahari yanaweza kutolewa katika sehemu tat. Sehemu ya kwanza ni wakati wa kuuliza, kupokea au kupekeka mahari.
Fanani – Gila Mkama
Hadhira – Gila Umwani
Fanani – Randaho ndo Mulandura
Tafsiri
Naomba kuruhusiwa kujigamba. Mimi ni gugu, ukiota juu yangu nakung’oa, upande mwingine wa majigambo ni wakati ambapo kuna makubaliano katikati ya mwanaume na mwanamke pale ambapo mahari imeshatolewa hivyo mwanaume na kundi lake wakiwa wamekaribia kufika nyumbani hujigamba kwa sauti kubwa ili waliobaki nyumbani ajue amefaulu na amekubali kuoa.
Mfano
Fanani: Nchnkorokoro,
Wote: Ulinde
Fanani : Nchkorokoro.
Wote : Ulinde
Mfano 5 Fanani:-
Nchkaruta kuruta bose,
Nchchijiji gi hita mugiteme,
Kandi gifatwa ntigifatike,
Ndumugunga gutuvingwa,
Ndigisaka mutinjigwa,
Abhogejeje kuchinjila bhanezayo,
Umuheto numwampi wanje ntibihusha.
Uhakana naze ndamubhome.
Aliho?
Wote: Ntawalihooo!
Kasha hufuatwa wimbo baada ya majigambo haya; ambazo ni:-
Fanani; Ni ya nzobe mubhilonge
Wote: Ni ya nzobe mubhilonge
Tafsiri
Fanani: Mimi ni shujaa
Wote: Wewe ni nani?
Fanani: Mimi ni shujaa
Wote: Wewe ni nani?
Fanani: Mimi ni zaidi kuliko wote,
Mimi ni kivuli kifikacho motoni kisiungue,
Tena kishikwacho kisishikike,
Mimi ni mchongoma usiokwewa,
Mimi ni msitu usioiingilika,
Waliojaribu au waliothubutu kuingia hawakurudi,
HITIMISHO
Kwa kuhitimisha, ni dhahiri kuwa majigambo na malumbano ya watani yanaweza kufifia kwa kiasi Fulani katika jamii pengine hii hutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia katika jamii nyingi ikiwa ni pamoja na usikilizwaji wa santuti (muziki) bali maendeleo ya sayansi na teknolojia kamwe hayawezi kathiri umuhimu wa majigambo na marumbano ya watani hii ni kutoka na kuwa jamii hizi hubeba ujmbe mzito wenye kuonya, kusisimua hata kuamsha hali ya uzalendo pengine kuliko santuti penwa au muziki ya kisasa ambayo kwa mtazamo inaenea kwa kiasi zaidi kuliko jamii nyingine.
MAREJELEO
Collins K.M na Ngamia F.O (2004), Johari ya Kiswahili, kidato cha tatu, East African
Educational Publishers, Nairobi, kampala, Dar es Salaam.
Mulokozi M.M (1989), Tanzu za Fasihi Simulizi, Mulika. Dar es Salaam TUKI
Mulokozi M.M (1996), Fanani ya Kiswahili, Chuo Kikuu Huria cha Dar es Salaam
Nimebadilika (2011), Dardanus Mfalme, Printed in the United State of America
Sanyamunza C.A (2014), Misingi ya Kazi za Kubuni, Nadhuna, Mbinu na mfano
kazi Bunilizi, Kanjamer print Technology
Wamitilia K.W (2002), Uhakiki wa Fasihi Misingi na Vipengele vyake, Nairobi
Phoenix
Wanjara F.S (2013), Kitovu cha Fasihi Simulizi kwa shule, Vyuo na ndaki, Serengeti Educational Publishers (T) LTD Mwanza – Tanzania