Uongozi wa ligi ya Italia, Serie A umepata ukosoaji mwingi baada ya kuzindua kampeni yao ya kupinga ubaguzi wa rangi ikiambatana na michoro ya nyani watatu
Ligi hiyo imesema michoro hiyo imelenga kuonesha, usambaa kwa thamani ya ushirikiano,tamaduni nyingi na undugu.
Bodi ya kupinga ubaguzi wa rangi barani Ulaya Fare, imepinga vikali kitendo hicho cha kutumia nyani katika kampeni hiyo na kuonesha kuchukizwa na kitendo hicho
“Kwa mara nyingine tena soka la Italia limeiacha dunia haina la kusema, ni vigumu kuona kipi Serie A walikuwa wanafikiri,nani aliwashauri," ilieleza taarifa ya Fare
Pamoja na hayo wadau mbalimbali pamoja na mashabiki wa kandanda wamestaajabishwa na kitendo hicho.