Karibu katika maswali kadhaa ya ushairi ambayo yatakusaidia kujiandaa na mitihani.
**Mashele Kiswahili.
1. Mshairi ni askari jadili kwa kutumia diwani mbili ulizosoma.
2. Mshairi hakurupuki, Bali hujadili kwa kina masuala mazito ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. Thibitisha hoja hii kwa kutumia diwani mbili huku ukishadadia ushahidi wako kwa hoja na mifano.
3. Mashairi hayana nafasi katika karne ya 21 jadili
4. Jadili historia ya ushairi wa kiswahili.
5. Chimbuko la ushairi wa kiswahili ni uarabu na kiarabu jadili.
6. Mshairi ni Mwalimu jadili kwa kina.
7. Eleza na fafanua aina za ushairi.
8. Ushairi ni kitulizo cha moyo, wenye kujaa ufundi, na matumizi makubwa ya lugha jadili.
9.
Fafanua kwa hoja tatu kutoka kila diwani kati ya mbili ulizosoma ni kwa jinsi gani wasanii wa kazi hizo wamefanikiwa kuzungumzia suala la mapenzi katika jamii kwa namna tofauti.
10.
Matumizi ya lugha ni nyenzo muhimu katika kufanikisha azma ya msanii kufikisha ujumbe kwa jamii. Thibitisha kauli hiyo kwa kutumia diwani mbili kati ya ulizosoma. Toa hoja tatu toka kila diwani.
11
Nafasi ya mwanamke ni jambo ambalo limekuwa likizungumziwa sana na wasanii wa kazi za fasihi. Toa hoja tatu kutoka kila diwani kuonesha jinsi wasanii wa kazi hizo walivyomtweza na kumkweza mwanamke kupitia kazi zao.
12
Suala la ukombozi wa kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni ni miongoni mwa dhima za kifasihi ambazo waandishi wa diwani wameibua ndani ya kazi zao ili kujenga jamii mpya. Thibitisha dai hilo kwa kutoa hoja tatu kutoka kila diwani kati ya mbili ulizosoma.