Mara nyingi ganzi hutokea endapo kuna michomo au mgandamizo wa mshipa wa fahamu. Magonjwa aina Fulani kama kisukari huweza kuharibu mishipa mirefu ya fahamu mwilini kama inayopeleka hisia kwenye mikono na miguu na pia huweza kusababisha miguu kupata ganzi.
Mara nyingi ganzi hutokea kwenye maeneo yaliyo mbali kutoka katikati ya mwili, mfano mikono na miguu. Unapopata ganzi mara nyingi haimaanishi kuwa unashida kubwa ndani ya mwili wako kama vile kiharusi au saratani.
Mara utakapofika hospitali daktari atachukua historia ya tatizo lako ili kujua kisababishi ni nini pamoja na kufanyiwa vipimo vya utambuzi kulingana na historia yako na shida anayohisi kwa asilimia nyingi kwamba utakuwa nayo.
Baadhi ya visababishi vinavyofahamika kuleta tatizo la ganzi ni pamoja na;
Magonjwa kwenye ubongo na mishipa ya fahamu yake mfano;
- Neuroma ya akaustik
- Anurismu ya ubongo(kuvimba kwa mishipa ya damu ya ubongo)
- Fistula kati ya mshipa wa arteri na Vein kwenye ubongo
- Saratani ya ubongo
- Ugonjwa wa Guillain Bare sindrome
- Paraneoplastik sindrome
- Jeraha kwenye mishipa ya pembeni ya mwili
- Jeraha kwenye uti wa mgongo
- Saratani kwenye uti wa mgongo
- Kiharus/stroke
- Kiharusi cha mpito
- Michomo kwenye kuta za maelini
Majeraha au tatizo la kutumika sana kama;
- Jeraha kwenye pleksasi ya brachial
- Sindromu ya kapal tuneli
- Kuungua na barafu
Magonjwa sugu
- Tatizo la kutumia pombe kupindukia
- Ugonjwa wa amailoidi
- Ugonjwa wa meno wa charcot Marie
- Ugonjwa wa Fabrys
- Ugonjwa wa sclerosis iliyosambaa
- Ugonjwa wa Pofria
- Ugonjwa wa Reinaudsi
- Tatizo la sjogrens
Magonjwa ya Maambukizi
- Ukoma
- Ugonjwa wa laimu
- Maambukizi ya kirusi cha Herpes zoster
- Ugonjwa wa Kaswende
Madhara ya dawa
- Dawa za kutibu saratani na UKIMWI
Visababishi vingine
- Kutumia madini mazito
- Kuvimba kwa mishipa ya damu ndani ya kifua
- Michomo ya kwenye mishipa ya damu
- Upungufu wa Vitamini B-12
Mwone daktari haraka endapo
- Ganzi imeanza ghafla
- Imetokana na kupata jeraha kichwani
- Ipo kwenye mkono mzima au mguu mzima
- Endapo inaambatana na kupooza au kuwa dhaifu kwa sehemu ya mwili
- Kuchanganyikiwa
- Shida kuongea
- Kizunguzungu
- Maumivu makali ya kichwa nay a ghafla