Serikali imetoa fursa kwa wanafunzi waliofaulu kidato cha nne mwaka 2019 na wanaotegemea kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo kwa mwaka 2020 kubadilisha Tahasusi(Combination) au kozi ,kuanzia 25 Machi 2020 hadi tarehe 19 April ,2020 kabla zoezi ya kuwapangia shule na vyuo kuanza.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo Zoezi hili la kujaza Tahasusi na kuchagua vyuo limeanza kutekelezwa mwaka jana na hii ni mara ya pili kufanyika ambalo linafanywa kwa njia ya mtandao,na linafanyika kabla ya kuwapangia vyuo au shule (Selection).

Ukiwa kwenye internet, fungua kivinjari chako (browser mfano, chrome), andika anuani ifuatayo selform.tamisemi.go.tz kupata dirisha la kujaza taarifa zako za kujisajili.

Waziri amesema kabla ya uamuzi huo wanafunzi wengi wamekuwa wakikosa nafasi za masomo kwasababu tu tahasusi au kozi walizochagua kabla ya matokeo zote zimekataa hivyo utaratibu huu mpya walioutoa wa kuchagua baada ya matokeo utatoa fursa sawa kwa wote na kuondoa malalamiko.