Thursday

Kijana Huyu ni nani haswa? Mjue kijana huyu ambaye picha yake imekuwa ikionekana sana katika mitandao ya kijamii

0 comments


   
Picha zake zimekuwa zikitumika sana katika mitandao ya kijamii.



Jina lake halisi anaitwa Oladee kijana mzaliwa wa Nigeria. kwa sasa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Ilorin kinachopatkana eneo la Kwara nchini Nigeria.

Mwaka 2009 Oladee alipata mkasa mkubwa ambapo badae mkasa huo ukamfanya kuwa mtu maarufu sana duniani.

Mwaka 2009 alipewa kiasi cha Naira200 na bibi yake kwa ajili ya kununulia mahitaji ya chakula cha usiku,ikabidi aongozane na rafiki yake kwenda sokoni kwa ajili ya kufanya manunuzi hayo, lakini wakiwa Njiani walipita sehemu ya kucheza kamari/ bet na rafiki yake akamshawishi ili waizalishe ile hela N200.

Kwa bahati mbaya hela yote waliyopewa ikaliwa kwenye kamari (bet), hiyo ndio hapo sasa bwana Oladee alipoanza kulia ili arudishiwe hela yake.

2354931_1585717183987.png

Alilia kwa hisia kali sana akikumbuka nyumbani bibi yake atamwadhibu hivyo alijaribu kumsawishi aliyemla arudishe hela yake bila mafanikio.

Kwa sasa Oladee yupo chuo kikuu na bado anajishughulisha na kuchekesha na kurekodi video fupi fupi, lakini analalamika kuwa hafaidiki na kile kinachotumika mitandaoni kama Facebook, Instagram na hata WhatsApp anatumika kama stickers lakini hakuna anachofaidika nacho.

Watu wanamwita kichwa kinachotembea bila passport kwa sababu picha yake hii imesambaa dunia nzima na watu wanai edit kwa kuifanyia vituko.
 

2288385_FB_IMG_1580273072675.jpeg

2288386_FB_IMG_1579984681596.jpeg
 

2288388_FB_IMG_1580273070356.jpeg

No comments:

Post a Comment