Watu 150 waripotiwa kufariki katika jimbo la Kano kwa maradhi yasiojulikana nchini Nigeria.
Mkurugenzi huyo amesema kwamba vifo hivyo vimetokea kati ya Ijumaa na Jumapili wiki iliopita.
Daktari Isa Abubakar amefahamisha kuwa watu waliofariki ni watu wenye umri wa kuanzia miaka 60.
Daktari huyo amewaambia wanahabari kuwa huenda watu hao wamefariki kwa virusi vua corona kwa kuwa sio jambo la kawaida idadi kubwa ya watu kufariki kwa mkupuo.
Nchini Nigeria ni watu 22 ndio wamekwishafariki kwa virusi vya corona na wengine 665 wakiwa wamekwishaathirika na virusi hivyo.