Saturday

The Last Thing He Wanted”: Filamu inayokusubiri wikiendi hii

0 comments

  • Ni filamu inayomhusu mwandishi wa habari anayejulikana kama Ellie.
  • Wakati akifanya habari za kiuchunguzi anajikuta akiangukia chini ya macho ya wasiopenda kufuatiliwa.
  • Kufiwa na baba yake, kunusurika kufa, hofu juu ya mtoto na familia yake ni sehemu ya visa vya filamu hii.

Dar es Salaam. Elena McMahon ni mwandishi wa habari za uchunguzi anafanya uchunguzi juu ya biashara ya silaha inayofanyika nchini Marekani.
Wakati akichimba habari hiyo, anajikuta amejivika visivyovalika baada ya Richard McMahon ambaye ni baba yake kumhusisha na biashara ya silaha wakati akiwa kwenye siku za mwisho za maisha yake.
Ufukunyuku wa mwanadada huyo unamfanya adondokee kwenye rada za watu wasiopenda “wambea” kama yeye.
Familia iliyovunjika, baba anayeaga dunia, mtoto anayemlilia na kazi zinazomuelemea ni sehemu ya kimbembe kinachomsibu mwanadada huyu ambaye ni mwandishi mashuhuli wa habari.

    Ataweza kuishi endapo kila hatua yake iko chini ya uangalizi? Fuatilia filamu ya The Last Thing He Wanted katika mtandao wa Netflix ambapo utakutana na waigizaji maarufu wakiwemo Anne Hathaway, Willem Dafoe na Rosie Perez wakikungoja kukonga moyo wako.
    Kama filamu siyo fungu lako, wikiendi hii inaweza kuwa njema kwako kama utaamua kutoka mtoko na kupumzika nyumbani na familia.

    No comments:

    Post a Comment