Thursday

Akiwa na tabia hizi anafaa kuwa mke wako

0 comments

 Eric Omondi akiwa na wife material wake Carol



Tabia za mwanamke ambaye ni wa kuoa (wife material)

1. Anakusikiliza wakati unaongea.
Ijapokuwa hili linaonekana swala dogo, ikija kwa kuchagua mwanamke lina umuhimu mkubwa. Mwanamke ambaye anakusikiliza wakati unapoongea ni ishara kuonyesha kuwa anakuheshimu. Na heshima ndio msingi wa ndoa.

2. Anaingiliana na wengine kiurahisi.
Mwanamke wife material ni yule ambaye ni rahisi kwake kuingiliana na watu wengine bila tatizo. Hakasirishwi na mambo madogo madogo ambayo wengine wanaweza kumfanyia. Badala yake yuko tayari kukumbana na chochote ambacho atapitia akiwa anajumuika na wengine.

3. Anakushughulikia iwapo umekuwa mgonjwa.
Angalia mwanamke ambaye unadeti naye kwa sasa. Iwapo anataka starehe pekee na hashughuliki na wewe kama umekuwa mgonjwa huyo si wife material. 

4. Ana tabia za kimama.
Mwanamke unayedeti kama anapenda watoto wa wengine na kuwajali ni ishara nzuri kuwa atakuwa na hulka nzuri za kimama. Hivyo iwapo anapenda watoto wa wengine, wako atawapenda zaidi.

5. Anakuwa na uamuzi huru.
Wakati unatafuta mwanamke wa kuoa, hakikisha mwanamke huyu anakuwa na uamuzi wake binasfi. Usikubali kuoa mwanamke ambaye kila kitu ambacho anataka kufanya lazima akuulize wewe.

6. Haabudu pesa.
Mwanamke wife material ni yule ambaye hana tamaa ya pesa. Ndoa huwa zina changamoto zake. Hivyo kama mwanamke uliye naye amezoea pesa basi ule wakati pesa zitatoweka naye pia atakutoka.

7. Anawapenda marafiki zako.
Mwanamke aina hii huwa anawathamini sana marafiki zako. Hii ni muhimu kwa kuwa anajua thamani ya marafiki zako.

8. Anakusaidia ufanikiwe maishani.
Sifa nyingine za mwanamke ambaye ni wife material ni kuwa yuko tayari kukujenga kimawazo ili uweze kufanikiwa kimaisha. Ukiona mwanamke hata hajui kazi unayofanya achana naye huyo hakufai.

9. Anaficha udhaifu wako.
Kila mtu anakuwa na udhaifu wake kwa njia moja au nyingine. Hivyo mwanamke ambaye ni wife material akiutambua udhaifu wako hawezi kukutenga bali atafanya kila juhudi kuhakikisha unakabiliana na udhaifu huo hadi unafaulu.

10. Yuko tayari kuvumbua mapya chumbani.
Ikija katika maswala ya chumbani, mwanamke ambaye ni wife material yuko tayari kuvumbua mambo mapya. Kama kifo cha mende kimewachosha mnaweza kujaribu daudi msalabani bila tatizo. 

11. Anaelewana na mamako.
Mwanamke wife material ni yule ambaye ukimpeleka kumtembelea mama yako anaelewana na yeye na wanakuwa marafiki. Ukiona anamkashifu mama yako kuwa hampendi basi huyo hakufai.

12. Familia yako inampenda.
Ukiona ya kuwa kila mtu katika familia yako hakosi kumtaja mwanamke huyu mara kwa mara kwa nia nzuri, basi huyo amepitishwa na familia na ni wife material tayari.

13. Anaheshimu ndoto zako.
Mwanamke wife material ni yule ambaye yuko tayari kukusaidia kutimiza ndoto zako. Kama ana uwezo wa kusaidia kufanikisha kile ambacho unatamani kukitimiza maishani basi mwanamke aina hii ni wa kuoa.

Upo!!

Hizi ni baadhi ya tabia za wife material lakini kuna tabia nyingine nyingi ambazo unaweza kuongeza ili uweze kumtambua yule ambaye anakufaa

No comments:

Post a Comment