Tuesday

Breaking : RAIS SAMIA AMPENDEKEZA DK. PHILIP MPANGO KUWA MAKAMU WA RAIS

0 comments

 



 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amempendekeza Waziri wa Fedha Dk. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kinachofuata sasa ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuthibitisha jina lake katika kikao cha bunge kinachoendelea muda huu jijini Dodoma.

 Spika wa Bunge Job Ndugai amesema Rais Samia amepeleka bungeni jina la Dkt. Philip Mpango ili awe Makamu wa Rais na kwamba utaratibu wa kupiga kura unafanyika bungeni.

No comments:

Post a Comment