Saturday

FASIHI YA KISAYANSI

0 comments

 


Jump to navigationJump to search

Bunilizi ya kisayansi (kwa Kiingerezascience fiction, inayofupishwa kama sci-fi au SF) ni aina ya fasihifilamumichezo ya video au sanaa. Hutumia habari za sayansi na teknolojia kuwaza hali ya wakati ujao, usafiri katika anga, usafiri wa wakati, roboti na mengineyo.

Hadithi zake zinasimuliwa mara nyingi katika ulimwengu ambao ni tofauti na ya kwetu siku hizi. Mtungaji wake atawaza mara nyingi vifaa na sayansi ambayo haipatikani leo au hata haiwezekani. Mara nyingi hadithi zake huwaziwa kutokea katika sayari tofauti pamoja na kutokea kwa viumbe visivyo wa Dunia hii.

Katika tamaduni mbalimbali kulikuwa na waandishi waliowaza safari za kwenda mahali kama mwezini, kwa mfano Lucianus wa Samosata katika enzi ya Roma ya Kale. Lakini hali halisi fasihi hiyo ilianza tangu kupatikana kwa teknolojia ya kisasa na kutokea kwa mabadiliko ya haraka yaliyoshawishi waandishi kuwaza matumizi yake nje ya maarifa ya kawaida.

Kati ya waandishi wa kwanza wanaohesabiwa katika fani hiyo ni Mfaransa Jules Verne aliyewaza matumizi ya bunduki kubwa ili kurusha watu mwezini au H.G. Wells aliyewaza mashine ya kupeleka watu katika wakati tofauti, lakini aliwaza pia kupatikana kwa usafiri wa ndegemashine za vita kama kifaruruninga na vingine ambavyo vilikuwa havijagunduliwa wakati alipoandika.

Kati ya waandishi mashuhuri ni Isaac Asimovprofesa wa biokemia aliyetunga hadithi fupi nyingi za bunilizi ya kisanyasi akikumbukwa hasa kwa masimulizi yake kuhusu maadili ya roboti inayoweza kujitawala zinazoangaliwa hadi leo.

Waandishi mara nyingi hutumia SF kuelezea changamoto za siku zetu kwa kuzisimulia katika wakati ujao au sayari nyingine. Kwa njia hiyo wanalenga wasomaji watafakari mawazo yenye maana.

Marejeo

Kigezo:Library resources box

No comments:

Post a Comment