Thursday

Idadi ya vifo vinavyosababishwa na homa ya Lassa yaongezeka hadi 42 nchini Nigeria

0 comments

 




Idadi ya vifo katika janga la homa ya Lassa, ambayo ilienea kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu nchini Nigeria imeongezeka hadi 42.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Nigeria (NCDC), watu 6 zaidi walifariki kutokana na janga hilo.

Hivyo basi, idadi ya watu waliofariki kutokana na janga hilo tangu mwezi Januari imeongezeka hadi 42.

Wakati huo huo, kesi 191 ziligunduliwa katika majimbo ya Edo, Ondo, Kaduna, Taraba, Ebonyi, Plateau na Bauchi kufuatia janga hilo lililoathiri nchi.

Homa ya Lassa, ambayo inaonekana katika nchi nyingi za Kiafrika kama Mali, Togo, Ghana, Liberia na Sierra Leone, iligundulika kwa mara ya kwanza Nigeria mnamo mwaka 1969 katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa nchi.

Serikali ya Nigeria ilitangaza hali ya "dharura" nchini kutokana na homa ya Lassa mnamo mwaka 2019.

Wakati watu 129 walifariki mnamo mwaka 2019 kwa janga la homa ya Lassa, ambayo maambukizi yake yalionekana kuongezeka kati ya mwezi Novemba na Mei haswa wakati wa msimu wa kiangazi kila mwaka, zaidi ya watu 300 walifariki mwaka 2020 katika majimbo 29 ya nchi.

Ugonjwa huo ambao unaambukizwa kwa kinyesi cha panya, pia unaweza kusambazwa kati ya wanadamu na husababisha homa mbaya ya damu.

Maafisa wanaonya umma kuwa waangalifu juu ya usafi na kuepuka panya pamoja na wanyama wengine wa jamii hiyo.

No comments:

Post a Comment