Friday

MAGONJWA YA MOYO : MAMBO MUHIMU KUZINGATIA

0 comments



Maambukizi katika kuta za ndani za moyo (Infective Endocarditis)



Na Dr Norman Jonas

Ni kundi la magonjwa linalohusisha magonjwa yanayoathiri moyo na mishipa yake ya damu. Hujumuisha magonjwa yafuatayo

i. Magonjwa yanayoathiri mishipa ya damu ya moyo

ii. Magonjwa yanayoathiri misuli ya moyo

iii. Magonjwa ya valve za moyo

iiii. Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa

UKUBWA WA TATIZO LA MAGONJWA YA MOYO DUNIANI

➢ Muuaji namba moja — Magonjwa ya moyo na mfumo wa damu ndio chanzo namba moja cha vifo duniani

➢ Kwa mwaka 2015 pekee zaidi ya watu milioni 17.7 walifariki kutokana na magonjwa ya moyo na mfumo wa damu. Hii ni sawa na theluthi ya vifo vyote duniani

➢ Zaidi ya theluthi. ya vifo vyote vya vinavyotokana na ugonjwa wa moyo na mishipa ya damu hutokea ndani ya nchi zenye uchumi wa chini na uchumi wa kati

MAMBO AU VIHATARISHI VINAVYOONGEZA UWEZEKANO WA MTU KUPATA UGONJWA WA MOYO

i. Ugonjwa wa shinikizo kubwa la damu (Presha) hasa kama hautumii dawa na matibabu ya kudhibiti presha

ii. Ugonjwa wa kisukari

iii. MATUMIZI YA SIGARA: Hii ujumuisha uvutaji wa sigara,tumbaku na ugoro

iiii. LISHE MBAYA: Ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi,sukari nyingi,chumvi nyingi, lehemu nyingi na kutotumia mbogamboga na matunda.

v. Unywaji pombe

vi. Uzito au unene uliopitiliza

vii. Kutokufanya mazoezi

viii. Umri : Zaidi ya miaka 50

ix. Historia ya ugonjwa wa moyo kwenye familia

x. JINSI: Jinsia ya kuime hupata ugonjwa wa moyo mapema

DALILI ZA UGONJWA WA MOYO

i. Maumivu ya kifua hasa yanayotembea mpaka kwenye mabega, shingo au taya

ii. Moyo kwenda mbio (Moyo kudunda kwa nguvu isivyo kawaida )

iii. Uchovu uliopitiliza, mwili kuwa dhaifu na kuchoka haraka hata kwenye shughuri ndogo

iiii. Kukosa pumzi au kushindwa kupumua vizuri hasa unapolala chali

v. Miguu, uso na tumbo kuvimba na kujaa maji

vi. Tumbo kujaa, kichefuchefu na kutapika

vii. Kushindwa kulala vizuri hasa kushtuka usingizini kuhisi kama unakabwa na kukosa pumzi

Hizi ni baadhi ya dalili na mara nyingi mtu huanza kupata dalili wakati ameshaishi na ugonjwa kwa muda mrefu. Ni muhimu sana kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara.

JE UNAWEZA VIPI KUEPUKA UGONJWA WA MOYO AU KUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA MARADHI HAYA?

Wataalamu wa tiba tunakubaliana kuwa njia nzuri ya kupambana na magonjwa ya moyo ni kuzuia yasitokee. Ni muhimu watu kuchukua hatua kuhusu vihatarishi vya magonjwa ya moyo kama ifuatavyo

1.LISHE

Japo kwa mara ya kwanza lishe bora huonekana kama jambo gumu ila baada ya mwili mwili huzoea na kufurahia chakula kama kawaida

i. Punguza vyakula vyenye wanga na sukari nyingi

ii. Punguza vyakula vyenye mafuta mengi hasa yale yanayotokana na wanyama

iii. Punguza ulaji wa nyama nyekundu kama ng’ombe, mbuzi inashauriwa kiasi cha nyama tunachokula kisizidi nusu kilo kwa wiki

iiii. Ongeza matumizi ya nafaka zisizokobolewa kama ugali wa dona,ulezi na mtama

v. Ongeza. ulaji wa vyakula jamii ya kunde, mbogamgoga na matunda

2.MAZOEZI

Kiwango cha mazoezi kinachoshauriwa kufanya ni walau dakika 30 kila siku. Kukaa bila kufanya mazoezi wala shughuri yoyote huuweka mwili katika hatari ya kupata magonjwa ya moyo

3.DHIBITI MATUMIZI YA VILEVI (POMBE NA SIGARA)

Epuka matumizi ya vilevi kama sigara na pombe. Kama mtumiaji wa pombe unatakiwa upunguze kabisa mpaka kiwango kinachoruhusiwa kitabibu

4. DHIBITI TATIZO LA PRESHA NA SUKARI

Ni vyema kuzingatia ushauri uliopewa na daktari kuhusu presha au kisukari pia na kuzingatia matumizi ya dawa kama ilivyoshauriwa na daktari.

5. MIKAZO (STRESS) ZA MAISHA

Mkazo (STRESS) uliopitiliza huuweka moyo katika hatari ya kupata maradhi. Ni vyema kutafuta namna ya kukabiliana na msongo wa mawazo na mkazo

6. Jenga tabia ya kupima afya yako mara kwa mara


No comments:

Post a Comment