Habari, ndugu msomaji Leo tuangazie afya ya wanachuo. Katika makala hii utajifunza njia mbalimbali zitakazo kuweka salama ukiwa chuoni ili uweze kuendelea na masomo yako vyema.
- Epuka Ngono isiyosalama, nimuhimu kutumia Condom kwa kila tendo landoa ili kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa kama vile, kisonono, na HIV/IDS
- Jenga tabia yakucheki afya yako/zenu kabla ya kuingia katika uhusiano wa kimapenzi, hii itawaepusha Na magonjwa kama vile, Ukimwi, homa ya ini, na magojwa yanayoambukiza kwa kujamiiana.
- Epuka kushirikiana viatu, nguo nk hii itakuepusha na magonjwa ya fangasi na magonjwa mengine yangozi.
- Zingatia usafi, wa mwili, kinywa na meno, pamoja na kufanya nguo zako kuwa safi kila Mara
- Epuka kula sana Vyakula vyamafuta na vinavyotengenezwa kwa mafuta mengi.
- Fanya mazoezi kila siku, kunywa maji yakutosha pamoja nakula lishe lamili ili kuuweka mwili wako Sawa kukabiliana na magonjwa.
- Katika kipindi hiki cha Covid-19, zingatia kanuni zote zakujikinga na magonjwa huo ukiwa nipamoja na kuvaa barakoa, kunawamikono na maji tiririka na sabuni na kuepuka kusalimiana kwa mabusu na mikono miongoni mwa kanuni nyingine.
-Epuka msongo wa mawazo hasa pale unapokosana na mwenzi wako au kufanya vibaya darasani kimasomo.
-Epuka kuangalia mwanga wa bluu kwa muda mrefu (simu, TV, PC,)
-Pata muda wakutosha wakupumzika/kulala
Ukizingatia Haya yote Mungu atakujalia afya njema kwa muda wote uwapo chuoni
Asante.