Sunday

Wakurugenzi Wanane Kikaangoni

0 comments

 



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo anakusudia kuwasilisha majina manane ya wakurugenzi katika Mamlaka ya Uteuzi kwa hatua zaidi baada halmashauri zao kupata hati chafu.


Jafo alisema haya muda mfupi baada ya CAG kuwasilisha hati za ukaguzi kwa rais Samia suluhu Hassan leo hii katika Ikulu ya Chamwino.


"Kwakuwa Wakurugenzi wa Halmashauri Mamlaka yao ya Uteuzi ni Mhe. Rais, nitawasilisha majina yao ili wachukuliwe hatua kwa kadiri atakavyoona inafaa‘ amesema Jafo.


Jafo amewataka watendaji wote katika Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuendelea kuchapa kazi kwa uadilifu kwa lengo la kuwatumikia wananchi.


No comments:

Post a Comment