Akitoa mawaidha katika ibada ya mazishi ya ndug, Saimon yaliyofanyika katika Wilaya ya Rombo kijiji cha Shimbi, Padre Marunda wa parokia ya Kirokomu amewaasa vijana kuacha matendo maovu na kumrudia Mungu. Padre huyo aliyeongea kwa hisia kali aliwataka vijana kuachana na ulevi, ulaji wa mikokaa huku akiwarai kujiepusha na utafutaji wa fedha au mali kwa njia zisizo za halali.
Katika ibada hiyo ya mazishi iliyohudhuriwa na watu mbalimbali Marunda aliwataka vijana kuiga maisha ya uchamungu kama alivyoishi kijana Simon aliyepumzishwa leo. " Utulivu ulioonekana hapa leo unadhihirisha Simon alikuwa kijana wa namna gani" alisema Padre huyo.
Aidha kiongozi huyo wa kiroho aliwasihi vijana kushiriki katika ibada kwani ni kwafaida yao na maisha yao kiujumla. Vilevile aliwataka vijana kubadilika kutoka katika mienendo isiyofaa na kumrudia Mungu huku akionya watakaokaidi hali itakuwa mbaya zaidi. Na mwisho aliongoza maombi ya kuwaombea vijana wote.
"mtandao huu unatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mpendwa wao"