
SERIKALI ya New Zealand imeripoti kile inachoamini kuwa kifo cha kwanza kinachohusisha chanjo ya corona ya Pfizer. Bodi huru inayosimamia usalama wa chanjo nchini humo imesema kifo cha mwanamke huyo huenda kimesababishwa na na maumivu katika ya misuli ya moyo.
Pia, imesema kulikuwa na changamoto nyingine ambazo kuna uwezekano zilisababisha athari za chanjo kutokea. Waangalizi wa Ulaya wamesema kuwa ugonjwa huo ni nadra na kuwa faida ya chanjo ni kubwa zaidi kuliko athari mbaya za chanjo.
Taarifa rasmi kuhusu sababu ya kifo bado haijatolewa. Hatahivyo, Bodi inayoshughulikia usalama wa chanjo ya Covid-19 imesema kuwa maumivu ya misuli ya moyo huenda yalitokana na chanjo.
Hii ni kesi ya kwanza nchini New Zealand ambapo kifo kimehusishwa na chanjo ya Pfizer COVID-19. Wakati Kituo cha Ufuatiliaji wa athari mbaya kimepokea ripoti nyingine za vifo kwa mtu aliyepewa chanjo ya hivi karibuni, lakini hakuna taarifa ya kifo inayohushwa na chanjo.