Wednesday

Bwana Harusi Avunjika Mgongo Baada ya Kurushwa Hewani

0 comments


MWANAUME mmoja aliyekuwa akifanya sherehe ya ndoa yake na mkewe baada ya kufunga ndoa amevunjika mgongo baada ya marafiki zake kumrusha juu juu na kukwepa kumdaka kisha akaanguka chini.

 

Kisa hicho kimetokea katika harusi hiyo Kaunti ya Bihor, Kaskazini Magharibi mwa Romania ambapo imeelezwa kuwa bwana harusi huyo aliporushwa hewani mara ya kwanza, alidakwa lakini katika jaribio la pili aliangukia kichwa na kumsababishia jeraha makubwa.

 

Sherehe hiyo ya harusi iliendelea licha ya mkasa huo huku bibi harusi na familia zote wakiendelea kuwaburudisha wageni waliokuwepo ukumbini.

 

Baada ya tukio hilo, marafiki hao walimubeba haraka na kumuweka kwenye gari, hatua ambayo madaktari walisema ilifanya hali yake kuwa zaidi.

 

Daktari anayemtibu amesema; “Mgonjwa aliumia uti wa mgongo. Anaendelea vizuri japo pole pole. Amelazwa katika chumba cha kufanya upasuaji wa kichwa na wiki ijayo atafanyiwa uchunguzi zaidi.”

 

Hata hivyo, bwana harusi huyo mwenye umri wa miaka 31 amepanga kuwashtaki marafiki zake hao kwa kumfanyia kitendo hicho kibaya. Ameongeza kuwa ameshazungumza na wakili wake akitaka kuwashtaki marafiki zake kwa kumsababishia jeraha.

No comments:

Post a Comment