Friday

Sokwe Ndakasi Afariki Dunia

0 comments

 


Sokwe anayefahamika kwa jina la Ndakasi, aliyepata umaarufu kupitia picha iliyopigwa mwaka 2019 akiwa ameweka pozi katika ‘selfie’ na mhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya DR Congo, amekufa baada ya kuugua kwa muda mrefu akiwa na miaka 14.

 

Ndakasi amekufa akiwa mikononi mwa rafiki yake, Mhifadhi Andre Bauma katika hifadhi ya Virunga National Park nchini Congo ambapo ndipo sokwe huyo jike alikuwa akiishi na wenzake.

 

Andre Bauma alikutana na Ndakasi wakati mnyama huyo akiwa na umri wa miezi miwili pekee (mwaka 2007) wakati akiomboleza msiba wa mama yake mzazi.

No comments:

Post a Comment